Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiwasili mtaa wa Mlandege kukagua kiwanja cha nyumba ya Ghorofa kinacholalamikiwa na Wakaazi wa Mtaa huo kwamba kimevamia pia eneo la wazi linalotumika kwa shughuli za Kijamii.
Mmiliki wa Kiwanja cha nyumba ya Ghorofa Mlandege Bwana Anuari Abdullah akijitetea kupata kibali kinachomruhusu kuendeleza ujenzi wa nyumba yake.
Baadhi ya Wakaazi wa Mtaa wa Mlandege wakitafakari na kufurahia maamuzi yaliyochukuliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif ya kuzuia ujenzi wa jengo la Ghorofa kwa kukosa taratibu zinazozingatia Mji mkongwe wa Zanzibar.
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amemuagiza Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar { ZAWA } kufanya uchunguzi wa kina na kuwachukulia hatua za nidhamu kwa mujibu wa sheria watendaji wa Mamlaka hiyo wanaotumia dhamana yao katika kusimamia huduma za maji kwa njia ya kuwanyanyasa Wananchi.
Alisema zipo dalili za wazi zinazoonyesha kwamba baadhi ya Watendaji wa Mamlaka hiyo wanatekeleza majukumu yao ya kazi kwa kuendesha utashi wao binafsi zaidi wa kisiasa.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa agizo hilo wakati akiwapa pole Wananchi wa Shehia ya Dole Wilaya ya Magharibi “B” mara baada ya kukagua mifereji ya huduma za Maji safi na Salama ya wananchi wa Shehia hiyo ambayo ilikatwa na mengine kung’olewa kabisa vianzio vyake kufuatia operesheni iliyofanywa na watendaji wa Mamlaka hiyo.
Opereshi hiyo ya Tarehe 22 Oktoba iliyoathiri nyumba 24 zenye familia 22 ililalamikiwa na Wananchi hao kwa vile ilitekelezwa siku mbili tu kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Tarehe 25 Mwezi Oktoba mwaka huu ikionyesha wazi kuwa baadhi ya watendaji wa Mamlaka hiyo waliweka utashi wao wa Kisiasa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...