Frank Mvungi- Maelezo
Baraza la Taifa la Ujenzi limepokea migogoro 41 na kufanikiwa kuitafutia ufumbuzi katika
kipindi cha mwaka 2015 kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya Ujenzi nchini.
Hayo yamesemwa na Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Ujenzi Mhandisi Dkt. Leonard
Chamuriho wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam.
Akizungumzia majukumu ya Baraza hilo katika kutatua Migogoro inayojitokeza katika Sekta
hiyo, Mhandisi Chamuriho amebainisha kuwa migogogoro iliyojitokeza imekuwa ikitegemea
Ukubwa wa mradi, Hali ya eneo la mradi, Ubora wa kazi, uelewa wa vipengele mbalimbali vya
mkataba katika mradi husika na moja ya pande zinazohusika kukatisha mkataba.
Kakika kukabiliana na migogoro hiyo, Baraza hilo limekuwa likitumia njia mbalimbali ikiwemo
kutoa ushauri wa kitaalamu kwa pande zinazohusika katika mradi, kuwakutanisha wadau chini
ya Baraza, kuweka wahusika chini ya aliyetatua mgogoro husika.
Akifafanua, Mhandisi Dkt. Chamuriho amebainisha kuwa Baraza hilo limekuwa likitumia njia
hizo kutatua Migogoro katika sekta hiyo pale inaposhindikana wahusika wanaweza kwenda
mahakamani kama hatua ya mwisho katika kutatua mgogoro husika.
Pia alitoa wito kwa watanzania wote hasa wadau wa Sekta ya Ujenzi kuwa na uelewa mzuri wa
jinsi ya kutekeleza miradi ya ujenzi kwa kuzingatia Sheria na kanuni ili kuepuka Migogoro.
Baraza la Taifa la Ujenzi ni Taasisi ya Serikali iliyoanzishwa kwa mujibu wa sheria ya Bunge
namba 20 ya mwaka 1987 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2008.(National Construction
Council Act, CAP 162,R.E.2008) ambapo Baraza lilianza kufanya kazi tarehe 17 August 1981.
Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Ujenzi Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho
akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam kuhusu Baraza hilo lilivyofanikiwa
kutatua migogoro kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya Ujenzi nchini.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Ujenzi
Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho leo Jijini Dar es salaam kuhusu Baraza hilo lilivyofanikiwa
kutatua migogoro kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya Ujenzi nchini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...