BELAKING of the Best Melodies, Christian Bella ‘Obama’.

KING of the Best Melodies, Christian Bella ‘Obama’ anatarajiwa kufunga mwaka (Desemba 31) na wimbo alioufanya na mkongwe wa muziki kutoka Kongo (DRC), Koffi Olomide uitwao Acha Kabisa, ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar. Akizungumza na mtandao huu, Bella anayetamba na Wimbo wa Nashindwa alisema usiku huo mashabiki watafunga mwaka kwa kuimba na kucheza ngoma zake zote kali kama vile Nani Kama Mama, Nakuhitaji, Msaliti, Nashindwa, Amerudi na nyingine kibao. 

 “Usiku huo nitafunga mwaka na kufungua mwaka mwingine nikiwa na bendi yangu ya Malaika Music huku tukitoa sapraiz kwa mashabiki wetu wote, pia kwa mara ya kwanza nitawaonjesha Wimbo wa Acha Kabisa niliofanya na Koffi Olomide pamoja na kutambulisha wimbo wangu mpya mwingine,” alisema Bella. Mashabiki pia wategemee kupata sebene la aina yake kutoka kwa Malaika itakayokuwa na vichwa kama Adaya, Petit Mauzo, Pilu, Mico Bella, Chesco Vuvuzela, Yanick Soslo, Babu Bomba, Kadogoo Machine na wengine wengine wengi. 5_5
Baada ya kufunga mwaka, katika Sikukuu ya Mwaka Mpya (Januari 1), bendi kongwe ya muziki wa Dansi, The African Stars ‘Twanga Pepeta’ ikiongozwa na Ali Chocky itakuwa na kazi moja ya kulishambulia jukwaa kwa kutoa sebene la kisasa. Akizungumzia shoo ya kufungua mwaka, Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo alisema kuwa siku hiyo pazia la burudani litafunguliwa mapema kuanzia asubuhi kwa kutoa nafasi kwa watoto wote kusherehekea kuukaribisha mwaka mpya. 

 “Tutakuwa na kundi linalotikisa kunako miondoko ya sarakasi na mazingaombwe kwa watoto la Masai Warriors ambapo watatoa burudani zote bila kusahau watoto wote wataburudika na michezo mingi kama vile kuogelea, kuteleza, kubembea pamoja na kucheza ndani ya ndege maalum,” alisema Mbizo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...