Benki ya Exim Tanzania imetangaza kufunga
mauzo ya dhamana yake ya muda mrefu (hati fungani) huku ikibainisha kuwa kiasi kilichopatikana
kutokana na mauzo ya hati hizo kimezidi mara dufu (asilimia 195) ya malengo ya
awali.
Kwa mujibu wa
taarifa iliyotolewa na benki hiyo jijini Dar es Salaam jana, uuzwaji wa dhamana
hizo ulifungwa rasmi Disemba 18 mwaka huu huku benki hiyo ikifanikiwa kukusanya
kiasi cha sh bilioni 19.7 kutokana na mauzo ya dhamana hiyo tofauti na
makadilio ya sh. bilioni 10 iliyokuwa imejipangia kukusanya hapo awali.
“Awali lengo letu
lilikuwa ni kukusanya takribani kiasi cha bilioni 10 hadi bilioni 15.
Tunashukuru kuona kwamba tulichokusanya ni karibu asilimia 200 ya malengo yetu
ya awali na kiasi kilichopatakina kimetoka kwa wawekezaji mbalimbali kutoka
kila kona ya nchi,’’ alibainisha, Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki hiyo, Bw.
Selemani Ponda.
Kupitia dhamana
hiyo wawekezaji wanapatiwa uhakika wa kupata riba ya 14% kwa mwaka
isiyokuwa na makato ya kodi,itakayolipwa kila baada ya miezi 6 kwa
kipindi cha miaka 6 huku ikiruhusu
wawekezaji wenye kiasi cha kuanzia shilingi milioni moja.
Akizungumzia zaidi
mafanikio hayo Bw Ponda alisema yametoa fursa kwa watanzania kuwa sehemu ya
ukuaji wa benki hiyo huku akiongeza;“Mafanikio haya yanaonyesha imani kubwa
waliyonayo watanzania kwa benki ya Exim na zaidi wanavutiwa na ubunifu wa benki
hii katika huduma za kifedha.,’’
Bw Ponda alitumia
fursa hiyo kuwashukuru baadhi ya wadau ikiwemo Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na
Dhamana nchini (CMSA), Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Wakala wa mauzo ya
dhamana hiyo, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) pamoja na wawekezaji wote kwa
kufanikisha mchakato mzima wa mauzo ya dhamana hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...