Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na Manispaa za jiji la Dar es salaam zitafanya zoezi la kuondoa wavamizi maeneo yote ya Mabondeni, kingo za mito na za Bahari, maeneo ya wazi, maeneo ya miundombinu na maeneo yote hatarishi zaidi ya 150 katika jiji la Dar es salaam. Bomoa bomoa ya leo inaendelea katika Bonde la mto msimbazi.
Mkuu wa Kitengo cha Sheria Balaza la Taifa la usimamizi wa mazingira Tanzania (NEMC), Manchale Heche akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam juu ya zoezi la Bomoabomoa maeneo ya miundombinu na maeneo yote hatarishi nakuwataka wananchi waliojenga katika fukwe za bahari Kingo za mito na mikondo ya bahari kuhamisha mali zao mapema.

Ng`ombe wa masikini hazai, akizaa, anazaa fahali!
ReplyDeleteHuwa kila siku najiuliza hawa jamaa wako wapi yote yakiendelea? Lkn wanaweza kupata ma doser ya kubomolea. sijui bajeti wanapata wapi maana ni maeneo mengi yanakumbwa. Wajiangalie kwa sababu hizo ni kazi za umma na lazima umma uwawajibishe. Sio kwa kubomoa bomoa, bali kuepusha hayo makosa!!!!
ReplyDeleteKwa ufupi hii haipendezi
ReplyDeletePia inaonyesha ni uzembe wa hao wanaohusika na usimamizi wa ujenzi. Kama kuna uvunjaji wa sheria katika kujenga sehemu hizo, kwa nini wajenzi hao hawakukamatwa na kupelekwa mahakamani hapo walipoanza tu kuweka misingi ya nyumba hizo haram? Kisha haitapendeza hapo kesho sehemu hizo hizo kujengwa na wenye pesa na mabavu.