Katibu Mkuu wa Chama Cha
Mapinduzi ( CCM),Ndugu Abdulrahman
O.Kinana(Pichani) akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya Kamati Kuu ya
Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kuipongeza Serikali ya Awamu ya Tano chini ya
uongozi wa Rais,Dkt.John Pombe Magufuli,Makamu wa Rais,Mhe.Samia Suluhu Hassan
na Waziri Mkuu,Mhe.Kassim Majaliwa kwa kasi nzuri waliyoanza nayo katika
utekelezaji wa Ilani ya Chama hicho.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akifafanua zaidi jambo mbele ya waandishi wa habari leo Desemba 8, 2015, katika Ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Makao Makuu
ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam
Baadhi ya Waandishi wa Habari
wakiendelea kumsikiliza Ndugu Kinana alipokuwa akizungumza mbele yao mapema leo mchana jijini Dar.
Na Bakari Issa Madjeshi.
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeipongeza
Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais,Dkt.John Pombe
Magufuli,Makamu wa Rais,Mhe.Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu,Mhe.Kassim
Majaliwa Kassim kwa kasi nzuri waliyoanza nayo katika utekelezaji wa Ilani ya
Chama hicho.
Kutokana na Kikao cha Kamati Kuu ya
Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kilichofanyika Desemba 07,2015 jijini Dar es
Salaam chini ya Mwenyekiti wa CCM,Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania,Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,kikao hicho kilipokea taarifa juu ya
utendaji wa Serikali katika utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka
2015-2020.
Akitoa pongezi hizo kwa niaba ya
Chama,Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu
Abdulrahman O.Kinana amesema Kamati Kuu imeunga mkono hatua zinazochukuliwa
na Serikali ya Awamu ya Tano katika kuhakikisha Ilani ya Uchaguzi ya Chama hicho kwa mwaka 2015-2020 inatekelezwa
kwa ufanisi.
Pia,Kinana amesema Kamati Kuu ya Chama
inapongeza na kuunga mkono juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali katika kusimamia
vyanzo vya mapato ya Serikali ikiwa ni kuhakikisha Mamlaka ya Mapato(TRA) na
Mamlaka ya Bandari Nchini(TPA) zinasimamia ukusanyaji wa kodi za Serikali
ipasavyo.
Hata hivyo,Ndugu Kinana amesema pamoja
na kuunga mkono na kupongeza kasi
waliyoanza nayo,Rais Magufuli,Makamu wa Rais na Waziri Mkuu,Kamati Kuu inawataka viongozi wengine wote kuiga
mfano huu mzuri na kuhakikisha wanatimiza wajibu wao ipasavyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...