Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASCO), limetangaza tatizo la upatikanaji wa huduma ya Maji katika maeneo yote yanayohudumiwa na mtambo wa kuzalisha Maji wa Ruvu chini pamoja na baadhi ya maeneo ya Mji wa Bagamoyo mkoani Pwani kutokana  na mtambo huo kuzimwa kwa wastani saa 24 siku ya Jumapili tarehe 13/12/2015.

Sababu ya kuzimwa kwa mtambo huo ni  kuruhusu kufanya matengenezo na maboresho ya njia kubwa ya Maji inayohudumia eneo la Salasala na viunga vyake vyote.

Akiongea na Waandishi wa habari jijini Dar es salaam Kaimu Meneja uhusiano wa Dawasco, Bi. Everlasting Lyaro, ametoa wito kwa wateja na wananchi  wote kuhifadhi Maji ya kutosha na kuyatumia kwa matumiz ya muhimu ili kuweza kukidhi mahitaji husika kwa kipindi hicho.
“Tupo katika maboresho ya huduma ya Maji, mtambo wetu wa Ruvu chini utazimwa kwa takribani saa 24, tunawaomba wateja wetu muhifadhi Maji ya kutosha na kuyatumia vizuri mpaka maketengezo yatakapokamilika, nasi tutajitahidi kadri tuwezavyo kuhakikisha tunarejesha huduma ya Maji kwa wakati uliopangwa” alisema Bi. Lyaro

Amebainisha kuwa matengenezo hayo  yatasababisha maeneo mengi  ya Jiji la Dar es Salaam kukosa huduma ya Maji ikiwemo Mji wote wa  Bagamoyo, Bunju, Boko, Tegeta, Kunduchi, Salasala, Jangwani, Mbezi beach na Kawe, Mlalakuwa, Mwenge, Mikocheni, Msasani, Sinza, Manzese, Mabibo, Kijitonyama, Kinondoni, Oysterbay, Magomeni, Upanga, Kariakoo, City Centre, Ilala, Ubungo Maziwa, Kigogo, Mburahati, Hospitali ya Muhimbili pamoja na eneo la Buguruni.

Everlasting Lyaro
Kaimu Meneja Uhusiano
022 2194800 / 0800110064

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...