Timu kabambe ya soka ya E-FM imeufunga mwaka kimichezo kwa kipute cha dakika 90 za mpira wa miguu dhidi ya maveterani wa Boko Beach katika uwanja wa Boko Beach jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.
E-fm ilifanikiwa kutawala mchezo katika kipindi cha kwanza na kuweza kuzitandika nyavu za Boko Beach Veterani mara mbili.
Kasi ya mchezo ilibadilika katika kipindi cha pili baada ya E-FM kuandika bao lake la tatu kupitia nyota wake John Makundi. Bao hilo liliamsha kikosi cha Boko Beach Veterani kwa kuutumia vizuri mpira wa adhabu kwa E-FM kujipatia bao la kufutia jasho lililofungwa na mchezaji wake Kudra Omar. Na hadi mwisho wa mchezo E-FM waliibuka wababe kwa jumla ya magoli 3-1
Picha ya pamoja ya kikosi cha E-fm
Picha ya pamoja ya kikosi cha cha Boko Beach Veterani
Ibrahim Masoud Maestro akiambaa na mpira
Mlinda mlango wa Boko Beach Veterani akijaribu kuwapanga walinzi wake
![]() |
Nahodha wa Efm Ssebo akitoka nje ya uwanja baada ya kulimwa kadi nyekundu kwa rafu ya bahati mbaya |
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...