Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Mahmoud Kambona akizungumza kwenye harambee ya ujenzi wa shule ya sekondari ya taasisi ya masjid Nuuru ya Mji mdogo wa Mirerani ambapo zilipatikana zaidi ya sh16 milioni (kushoto) ni Imamu wa masjid hiyo Mohames Shauri na kulia ni Willy Mushi meneja wa mgodi wa Tanzanite Africa.
Mshairi wa mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Husna Hussein akimkabidhi mkuu wa wilaya hiyo Hashim Kambona, shairi alilolighani kwenye chakula kilichoandaliwa na Mwenyekti wa IPP Dk Reginald Mengi na harambee ya kuchangia shule ya sekondari ya taasisi ya Masjid Nuuru.
Willy Mushi ambaye ni Meneja wa mgodi wa Tanzanite Africa Ltd unaomilikiwa na Mwenyekiti wa mtendaji wa IPP, Reginald Mengi akizungumza kwa niabaya Mengi aliyeandaa chakula na waumini wa eneo hilo na kutoa ahadi ya ujenzi wa madarasa mawili na ofisi moja ya shule ya sekondari ya taasisi ya masjid Nuuru ya mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro.
Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Mahmoud Kambona (katikati) akiwasili kwenye taasisi ya masjid Nuuru iliyopo mji mdogo wa Mirerani ambapo aliongoza harambee ya ujenzi wa shule ya sekondari na kupatikana zaidi ya sh16 milioni.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...