Jaji  Mkuu na Mwanasheria Mkuu Mstaafu, Mark Boman akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii 

JAJI Mkuu na Mwanasheria Mkuu Mstaafu, Mark Boman amesema kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Umoja Zanzibar, Maalim Seif Hamad akubali uchaguzi urudiwe Zanzibar kwani kama alishinda atashinda tena kutokana na waliompigia katika uchaguzi ulifutwa watampIgia kura tena.

Boman ameyasema hayo leo jijini Dar eS Salaam , wakati akizungumza na waandishi wa habari amesema kuwa Maalim kujitangazia kuwa ameshinda ni suala ambalo halikufuata utaratibu hivyo kutokana na mazingira hayo uchaguzi ufanyike ili kupata Rais wa Serikali ya Zanzibar.



“Kurudia uchaguzi Zanzibar ni jambo lisilo epukika lakini wakae na kuangalia dosari zilizojitokeza na kufuta uchaguzi lazima lishughukiwe kisheria bila kufanya hivyo kunaweza kuleta matatizo”amesema Jaji Mstaafu, Boman.


Amesema kuwa uchaguzi uliofanyika Zanzibar walitakiwa kukaa na kuona wapi walikosea katika kuondoa changamoto hizo ambapo ilikuwa ngumu kutokana na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Jecha Salum Jecha na wajumbe walishindwa kuafikiana.


Hata hivyo Boman ametaka suala la katiba lazima lishughulikiwe kuacha kwake ni aibu ya nchi kutokana na mabilioni ya fedha yametumika katika mchakato huo.


Amesema kuwa migogoro inayotokea ya ardhi na wafugaji pamoja wakulima inatokana na kutokuwa na katiba ambayo ndio ingekuwa suluhu ya utatuzi wa migogoro hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. wewe mzee kama ulikuwa huna lakuzungumza bora UNGEKAA KIMYA kuliko kucheuwa maneno yalokuwa hayana mpango

    na kwanini usimshauri shein akaondoka wakati dunia mzima inajuwa kuwa sio chaguo la wazanzibari hili suala kila mwenye akili zake timamu anajuwa kuwa ukitaka utende haki ni shein kutafuta sehemu ya kwenda akaondoka IKULU basi na sio vyenginevyo

    kaa kimya kama huna lakusema kama walivyokaa wengine nenda india kapimishe tena miwani yako kama bado hujauona ukweli mpaka hapo ulipofikia

    ReplyDelete
  2. Mheshimiwa angekaa kimya tu bila kusema chochote!! Maana, .... no comment!!

    ReplyDelete
  3. Hahahahahahahahaha .......dah wote tunajua kwamba jamaa walielekeza nguvu,akili na maarifa (la mkn) bara na kilichotokea visiwani ndio hiko kilichotokea. Kwa muda mrefu watu wameshajikusanya unapomshauri Maalim akubari hiyo ni sawa na ule mchezo wa zamani wa kipute yaani unamdanganya mtoto kana kwamba unampa zawadi/kitu akinyosha mkono unampiga kibao.Najua wapo wengi watakaojitokeza na ushauri kama huu wote si wema. Mshindi mbona anajulikana na jumuiya za kimataifa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...