Kituo bora cha radio 2015 E-fm leo kimekabidhi zawadi ya makapu yaliyosheheni bidhaa za vyakula kuelekea sikukuu ya Christmas Zoezi hili liliwataka wasikilizaji wa E-fm kusikiliza mlio wa Jingle Bells uliokuwa ukizunguka kwenye vipindi tofauti kisha kutambua muda ambao mlio huo umesikika, jina la kipindi husika na mtangazaji/watangazaji wa zamu waliokuwa studio muda huo. 
Akizungumza mara baada ya kukabidhi makapu hayo kwa washindi Meneja wa vipindi E-fm Bwana Dickson Ponela (Big Dad Dizzo) ameeleza kuwa, E-fm imekuwa ikishirikisha wasikilizaji wake kwa kuwapatia zawadi mbalimbali ikiwemo kuwawezesha kimaisha kama sehemu ya shukrani kwa kuichagua E-fm
Meneja wa vipindi E-fm Dickson Ponela akiwaonyesha washindi makapu ya sikukuu
Makapu ya sikukuu
Watatu kutoka kulia ni Dickson Ponela, wa kwanza kushoto ni Sendo kwenye picha ya pamoja na baadhi ya washindi
Mama Pili kutoka Gobgo la Mboto akipakia kapu lake kwenye Bajaji

Kaimu Mkurugenzi wa masoko na huduma kwa wateja NHC bwana Elisante Maleko akikabidhi kapu kwa mtoto Steve mkazi wa Kimara Suka aliyejishindia kapu la sikukuu
Patric Boniface kutoka Goba aliyeambatana na baba yake wakipakia mzigo wao kwenye bodaboda

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...