Na Nyakongo Manyama-Maelezo
Kesi inayowakabili wafanyakazi wa Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) inatarajiwa kusikilizwa tena January 13, 2016
Akizungumza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini dar es salaam Wakili wa Serikali Bi. Dianna Lukondo amesema kuwa kwa leo Kesi ilikuja kwa ajili ya kusikilizwa na kutoa dhamana kwa washtakiwa na hivyo imeshindikana kusikilizwa kutokana na upelelezi kutokamilika.
“Upelelezi haujakamilika hivyo kesi itasikilizwa tena Januari mwakani ” alisema Dianna.
Kesi hiyo inawakabili aliyekuwa Naibu Kamishna TRA Tiagi Masamaki, meneja wa kitengo Huduma kwa Wateja Habibu Mponezya, na wengine ni Khamis Omary, Eliaichi Mrema, Burton Kaisi, Harun Mpande na Raymond Louis.
Washtakiwa hao wanatuhumiwa kwa kosa la uhujumu uchumi, wakidaiwa kuhusika na upotevu wa makontena 329 katika Bandari ya Dar es Salaam yaliosababisha ukwepaji wa ushuru zaidi ya sh. Bilioni 80.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...