LUTENI KANALI (MSTAAFU) WILLY JOHN MASOI.
Sekunde, dakika, saa, siku, wiki, miezi imepita na leo ni mwaka tangu usiku ule ulipoitwa na Bwana Mungu na kutuachia uchungu usioelezeka. Pengo ulilotuachia kamwe haliwezi kuzibika bali tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwani kazi yake haina makosa na upendo uliotuachia ndio unatuwezesha kusonga mbele.
Tunaendelea kumuomba Mwenyezi Mungu akupumzishe kwa amani hadi hapo tutakapokutana kwani sisi wote ni wapitaji katika ulimwengu huu.
Tumebaki na kumbukumbu za imani yako iliyotukuka, mapenzi yako ya dhati, wema na ukarimu wako ambao hatutasahau daima. Tangu ile siku Bwana Mungu alipokuita kwenye ufalme wake tumekuwa na wakati mgumu kwa kuwa maisha yetu sasa hatuwezi kuyafananisha hata chembe na wakati tulipokuwa tunaisikia sauti yako, tunafurahi pamoja na kushauriana juu ya mambo mbali mbali ya familia zetu.
Unakumbukwa na mke wako mpendwa Mary Salome (Ndewioshindo), watoto, wakwe zako, wadogo zako, wajukuu, ndugu pamoja na majirani zako wote.
Raha ya milele umpe, ee Bwana, na mwanga wa milele uingazie roho ya marehemu Luteni Kanali (Mstaafu) Willy John" Masoi. Apumzike kwa amani" Amina
“NIMEVIPIGA VITA VILIVYO VIZURI, MWENDO NIMEUMALIZA, IMANI NIMEILINDA”
(2 Timotheo 4:7)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...