Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma,SSP Nuru Selemani akiwakiwaelimisha abiria ndani ya basi lilofanya safari zake mikoani ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa kampeni ya”Wait to Send”inayotoa elimu kwa madereva kutokutumia simu na kilevi wakati wote wakitumia vyombo vya moto.Kampeni hiyo inadhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Askari wa Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma SGT. Tunu Kuta(kulia) akimpima kiwango cha pombe mwilini dereva wa basi la kwenda mikoani, Masoud Seleman ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya”Wait to Send”inayodhaminiwa na Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na Jeshi la polisi kitengo hicho katikati Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani mkoa huo SSP Nuru Selemani na wapili kulia ni Kaimu mkuu wa kanda ya kati wa Vodacom Tanzania,Heladius Kisiwani.
Kaimu mkuu wa kanda ya kati wa Vodacom Tanzania,Heladius Kisiwani(kulia)akimpa maelezo dereva wa basi liendalo mikoani,Masoud Selemani kuhusiana na pete ya kidoleni inayotolewa na Kampuni hiyo kwa kushirikiana na jeshi la Polisi kitengo cha Usalama barabarani yenye ujumbe“Wait To Send” unaohamasisha madereva wa vyombo vya moto kutokutumia simu za mkononi wakiwa wanaendesha vyombo hivyo. Zoezi hili lilifanyika leo katika kituo cha mabasi yaendayo mkoani cha Dodoma.Katikati Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma,SSP Nuru Selemani.
Duh.. kweli bongo, kipimoja hiki hutumika wakati wowote kwa mtu yoyote akiwa njiani akiendesha gari. Fany kipaumbele kwa madereva wa mabasi uwezi kuwapima stendi ya bus. Wanatakiwa kuwa njiani mabasi yanakopita ndio wasimamishe basi na kumpima dereva. kumpima mtu stendi kama mchozo tu na pia madereva wanywaji huo wanakunywa njiani katikati ya safari huona kama wanatoa uchovu. Kwa hivi kupimwa stendi wanachezea tu roho za watu.
ReplyDelete