Na Pili Khatib na Zuhura Omar, MUM
Kuimarisha Zao la Karafuu ni sawa na kuimarisha Uchumi na Maendeleo ya nchi, jitihada za Wadau ni muihimu ili kufika lengo la Serikali la kuifanya Sekta ya Zao la Karafuu kuwa uti wa mgongo wa Uchumi liweze kufikiwa.
Kutokana na umuhimu wa Sekta ya Karafuu kwa Maendeleo ya Uchumi Serikali imefanya mageuzi makubwa katika sekta hiyo kwa lengo la kuongeza uzalishaji na tija kwa Wakulima na Taifa kwa jumla.
Katika utekelezaji wa Mageuzi hayo yaliyoanza mwaka 2011 Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar ZSTC ambalo ni mdau mkubwa katika uimarishaji wa Sekta ya Karafuu ilianzisha Mfuko wa Maendeleo ya Karafuu (Zanzibar Clove Fund) ambapo ulizinduliwa rasmi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein tarehe 28/08/2011.
Baadhi ya wafanyakazi wa ZSTC wakipita mbele ya Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohmaed Shein wakiwa wamebeba bango lenye ujumbe wa kuimarisha zao la karafuu.
Mfuko huo wa Maendeleo ya Karafuu umeanzishwa kwa mujibu wa Sheria mpya ya Maendeleo ya Karafuu Nam. 2 ya Mwaka 2014, chini ya kifungu Nam. 4 (1) ambacho kinaipa mamlaka Bodi ya Shirika la ZSTC kuanzisha Mfuko wa Maendeleo ya Karafuu. Mfuko huo upo chini ya Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la ZSTC.
Lengo kuu la kuanzishwa kwake ni Kuimarisha, Kuendeleza na Kusimamia Sekta ya Zao la Karafuu Zanzibar kwa kutoa msaada unaohitajika kwa Wakulima wa karafuu kwa lengo la kuongeza uzalishaji.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la ZSTC Mwanahija Almas Ali Sekta hiyo ya Karafuu inaendelea kuimarika zaidi hasa baada ya kuanzishwa kwa Mfuko huo wa Maendeleo ya Karafuu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...