WAIMBAJI nyota wa muziki wa Injili hapa nchini Martha Mwaipaja, Jesca BM na Christopher Mwahangila wanatarajia kupanda katika jukwaa la Tamasha la Krismasi linalotarajia kufanyika Desemba 25 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Waimbaji hao wanaungana na wenzao waliotangulia kuthibitisha kushiriki tamasha hilo ambalo lina mlengo wa kurudisha Shukrani kwa Mungu baada ya kufanikisha uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25 kwa amani na utulivu.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama aliwataja wengine ambao watakuwa sambamba na wenzao siku hiyo ni pamoja na Sifael Mwabuka sambamba na Kwaya ya Yombo KKKT.

Msama alisema tamasha hilo linadhaminiwa na gazeti la Dira ya Mtanzania ambako alitoa wito kwa mashirika na kampuni mbalimbali kujitokeza ili kufanikisha tamasha hilo.

Aidha Msama aliwataja wengine waliothibitisha kupanda jukwaa la tamasha hilo ni pamoja na Rebeca Malope, Eiphraim Sekeleti, Solomon Mukubwa, Faustine Munishi, Upendo Nkone, Christina Shusho, Joshua Mlelwa na Kwaya ya Wakorintho Wapili.

Msama anaweka bayana kauli mbiu ya tamasha hilo ni Njooni wote tumsifu Mungu kwa pamoja, tumuinue Mungu kwa nyimbo na kucheza mbele yake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...