Daktari Dhamana wa Kituo cha Afya Fuoni Said Fadhili Abass akizungumza wakati wa mkutano huo na Mbunge wa Jimbo la fuoni na kumshukuru kwa msaada wake huo kwa Kituo chao. na kusema dawa hizo zitatumika kwa wananchi wa Jimbo hilo wanaofika kituoni hapa kupata huduma mbalimbali za Afya.
Wauguzi wa Kituo cha Afya Fuoni wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Fuoni Mhe Abass Mwinyi wakati akizungumza na Wafanyakazi hao katika ziara yake kutembelea Kituo hicho na kukabidhi madawa kwa ajili ya Wananchi wanaofika kupata huduma kituoni hapo.
Mbunge wa Jimbo la Fuoni Zanzibar Mhe Abass Ali Hassaan Mwinyi akimkabidhi fedha shilingi milioni moja Dakt. Dhamani wa Kituo cha Afya Fuoni Zanzibar Said Fadhil Abass, kwa ajili ya kutatua makero zinazokikabili kituo hicho cha Afya Fuoni ili kufanya kazi zao kwa kuwahudumia Wananchi kwa ufanisi zaidi.Mbunge wa Jimbo la Fuoni Zanzibar Mhe Abass Ali Hassaan Mwinyi akimkabidhi madawa Dakt. Dhamani wa Kituo cha Afya Fuoni Zanzibar Said Fadhil Abass, kwa ajili ya matumizi ya kituo hicho kinachotowa huduma mbalimbali kwa Wananchi wa Fuoni zikiwemo za kuzalisha kinamama na upigaji wa vipimo vya utra sound katika kituo hicho na kulaza wagonjwa.
Mbunge wa Jimbo la Fuoni Zanzibar Mhe Abass Ali Hassaan Mwinyi akimkabidhi vifaa kwa akili ya vyoo vya kituo hicho Dakt. Dhamani wa Kituo cha Afya Fuoni Zanzibar Said Fadhil Abass na kulia Muuguzi wa Afya ya Jamii Kituoni hapo Mwaka Pandu Makame.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...