Mkuu wa Kitengo cha masoko kutoka GEPF Bw Aloyce Ntukamazina akiongoza timu ya wafanyakazi wa Mfuko pamoja na wafanyakazi wa Dangote kufanya usafi katika maeneo ya soko la Mbae na Ufukoni mkoni Mtwara katika kuadhimisha miaka 54 ya Uhuru wa Tanzania na kutekeleza agizo la Mh Rais John Pombe Magufuli la kuhakikisha watanzania wanafanya usafi katika maeneo yao.
Zoezi la kufanya usafi katika maeneo ya soko la Mbae na Ufukoni mkoni Mtwara likiendelea ikiwa ni katika kuadhimisha miaka 54 ya Uhuru wa Tanzania na kutekeleza agizo la Mh Rais John Pombe Magufuli la kuhakikisha watanzania wanafanya usafi katika maeneo yao.
Baada ya kumaliza usafi Mfuko wa GEPF uliandaa Bonanza maalum lililoshirikisha timu 3 kutoka katika KIwanda cha Dangote pamoja na timu ya wafanyakazi wa Mfuko wa GEPF. Lengo la Bonanza hilo ilikuwa kudumisha umoja na ushirikiano baina ya Dangote na Mfuko wa GEPF na Kauli mbiu ya Bonanza hilo ilikuwa "USAFI KWANZA BURUDANI BAADAE".
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...