Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Epharaim Kwesigabo akizungumza na waandishi wa habari juu ya mfumuko wa bei kwa mwezi Novemba ambao umefikia asilimia 6.6 leo jijini Dar es Salaam, Kushoto ni Meneja wa  Mfumuko wa Bei wa NBS , Ruth Minja.
 02.Waandishi wa habari wakifatilia taarifa kutoka Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu,Epharaim Kwesigabo  hayupo picha leo jijini Dar es Salaam.
(Picha na Chalila Kibuda wa Globu ya Jamii)
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza  Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Epharaim Kwesigabo jijini Dar es Salaam leo.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
MFUMUKO wa bei wa Taifa kwa  Novemba 2015 umeongezeka hadi asilimia 6.6 kutoka asilimia 6.3  ya Oktoba mwaka huu.
 
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Epharaim Kwesigabo amesema kuwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia Novemba.
 
Kwesigabo amesema mfumuko wa bei wa bidhaa ya za vyakula na vinywaji  Baridi  Novemba mwaka imeongezeka  kwa asilimia 11.2 kutoka asilimia 10.2 tofauti na mwezi uliopita.
 
Amesema kuongezeka kwa Mfumuko wa bei wa Novemba 2015  kumechangiwa na kuongezeka kwa baadhi ya bidhaa za vyakula kwa  kipindi cha mwezi uliopita zikilinganishwa na bei za Novemba mwaka jana.
 
Aliongeza kuwa mwenendo wa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula zilizoonesha kuongezeka Novemba 2015 ukilinganishwa na bei za Novemba 214  ni pamoja na mchele kwa asilimia 25.8, Mahindi asilimia 16.4, unga wa mahindi asilimia 12.0  nyama asilimia 8.7, Samaki asilimia 21.4, Mharagwe asilimia 14.5  Choroko asilimia 15.3 Mihogo asilimia 10.7  pamoja na viazi vitamu 23.4.
 
Kwesigabo amesema kuwa uwezo wa sh.100 katika kununua bidhaa na huduma umefikia sh.62.31 mwezi Novemba, 2015 kutoka Septemba 2010  ikilinganishwa na Sh. tofauti na Novemba mwaka jana sh.100 uwezo wake ulikuwa ni sh.62.82  ilivyokuwa Oktoba 2015.

Mfumuko wa bei  Afrika Mashariki,nchi ya Kenya  kwa Novemba imeongezeka kwa asilimia 7.32, kutoka asilimia 6.72 ya  Oktoba mwaka huu, Uganga imeongezeka hadi asilimia 9.1kutoka asimia 8.8 ya mwezi uliopita  hali hiyo inafanya nchi ya Uganda kuwa ya kwanza kwa kuongeza mfumuko wa bei.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...