Waziri wa Kilimo, Uvuvi na Ufugaji, Mwigulu Nchemba akiangalia Ng'ombe walio uwawa katika Mgogoro wa wakulima na Wafugaji uliotokea katika kijiji cha Dihinda kata ya Kanga wilayani Mvomero, katika tukio lililotokea Desemba 12 mwaka huu.
Waziri wa Kilimo, Uvuvi na Ufugaji, Mwigulu Nchemba akiwa na Mkuu wa wilaya ya Mvomero, Betty Mkwasa wakiwajulia hali watu waliojeruhiwa katika mgogoro wa wakulima na wafugaji uliotokea katika kijiji cha Dihinda kata ya Kanga wilayani Mvomero Desemba 12 mwaka huu.

Waziri wa Kilimo, Uvuvi na Ufugaji, Mwigulu Nchemba akizungumza na wanachi wa kijiji cha Dihinda waliokusanyika katika eneo lililotokea mauaji ya wanyama na baadhi ya watu kujeruhiwa.
"Natoa rai kwa Wananchi hususani wa jamii ya Wafugaji na Wakulima, kuwa hakuna ardhi au Mnyama mwenye thamani sawa na Maisha ya Mwanadamu yeyote yule, njia bora na salama ya kutatua migogoro hii inayohusisha wakuliama na wafugaji ni kufuata taratibu za kuonana na Uongozi wa Serikali wa eneo husika hatua kwa hatua, Nawaomba wananchi waache kujichukulia sheria mikononi, tunakwenda kuunda kamati za usuruhishi wa migogoro hii kwa kila kijiji zitakazohusisha pande zote mbili ili kubaini wavamizi wa maeneo na kuwachukulia hatua za kisheria." Alisema Nchemba.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...