Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwan J. Kikwete.

Ndugu zangu waandishi wa habari, nimeamua kuwaita ili kuzungumza nanyi kuhusu baadhi ya mambo yaliyokuwa yanasemwa katika vyombo vya habari kuhusu mimi.

Awali ya yote napenda kusema kuwa habari hizo ni UONGO mtupu, ni mambo yanayozushwa na waandishi wa habari hizo kwa nia ya kuchafua jina langu kwa sababu wanazozijua wanaoandika. UKWELI ni kwamba haya ni mambo yenye kufanywa kwa nia na dhamira mbaya dhidi yangu na hata familia yangu.

Hivi karibuni, kwa mfano, lipo gazeti moja liliandika na kutoa picha yangu na mtu mmoja waliyedai ni Mhe. Paul Makonda eti akinifunga kamba za viatu. Katika maelezo yake mwandishi akadai kuwa Mhe. Makonda alipata uteuzi kuwa Mkuu wa wilaya ya Kinondoni kwa sababu hiyo. Huu ni uongo usiokuwa na hata chembe ya ukweli. 

Napenda watanzania wajue kuwa hakuna wakati wowote Baba yangu alipokuwa Rais wa nchi yetu alinihusisha kwa namna yeyote ile katika uteuzi wa mtu yeyote katika Serikali. Hivyo basi kujaribu kunihusisha na uteuzi wa Mhe. Paul Makonda kuwa Mkuu wa Wilaya wa Kinondoni ni jambo lisilokuwa na ukweli wowote. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Labda kuna watu hakuishi nao vizuri ndiyo maana anaandamwa kiasi hiki. Au kuna watu waluchafuliwa na wanahisi ridhiwani anahusika basi na wao wameamua kumchafua.

    Kuna kauli ya kibaguzi aliwahi kuitoa Ridhiwani. Kauli hiyo ikaungwa mkono na Nape Nnauye. Halafu mbunge Nassary naye akajibu bungeni. Tukaja kusikia tena kwenye kampeni za Uraisi.

    Ridhiwani anapaswa kuomba radhi kwa kauli ile ya kibaguzi.

    ReplyDelete
  2. Pole mh ridhiwani. Tatizo ni ngumu kujisafisha kwa kinywa chako kwa sababu no one expects you to adimit any wrong doing. I would definitely expect you to come out and strongly defend yourself but unfortunately in won't mean anything in the public eye

    ReplyDelete
  3. To be honest huyu kijana wanamzushia sana na ni mambo ya aibu sana kwa watanzania, imagine uzushi eti alishikwa na unga china??Kweli??Na wajinga na wapumbavu tu ndio wanaoamini huu uzushi lakini kwa sisi wa ughaibuni hatuamini huu uzushi..Watu wanachosahau huyu kijana kabla hata baba yake hajawa rais alikua serikalini kwenye post mbalimbali na tena za juu kwa Zaidi 25 years..iweje eti aje awe rais ndo mtt wake abebe sijui unga...huu ni wivu wa kike na uzushi mbaya sana unaoenezwa kwa familia ya rais wetu mstaafu sio mzuri..nafikiri sharia ya mitandao ifanye kazi yake...pole Riziwani,sikujui na hunijui ila Napata hasira tu unavyozushiwa mambo ya kijinga na kipumbavu na watu wasiokutakia kheri,.
    Mdau wa UK

    ReplyDelete
  4. What is the point of calling a news conference to say the news papers were slandering you. Wapeleke mahakamani na wanyoe nywele.

    ReplyDelete
  5. Pole sana Mheshimiwa,
    Ila inanbidi uangalie kwenye kioo na kuona kuna nini. Kwanini unasakamwa wewe tu? Tumeona watoto wa Maraisi waliopita mbona hawakuwa wanasakamwa namna hii. Jamii nayo imekuwa ya kimtandao kila kitu kinaenezwa mtandaoni na kusambaa kwa kasi.
    Nomba uwachukulie hatua kali kama unajua kina nani wapo kwenye hili la kusambaza uongo kwa jamii yetu. Jamii inapoanza kuamini uongo ni mmongonyoko wa maadili. Inabidi jamii yetu irudi kwenye mstari na kuachana na mambo yasiyokuwa na tija kama hayo ya kuzushia watu uongo badala yake tujikite kuendeleza taifa letu.

    Asante.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Eh. Huyu nae anaona si kosa kumlaumu mkosewa. Kwa mwendo huu tutajikuta tunapoteza identity kwa kuwaridhisha wenye kuuchongabila kufata maadili. Lazima mtu akatae kuyumnishwa ni midomo ya watu.

      Delete
  6. People blaming the victim. Why do you even have to defend? The burden of proof is always on the accusor. Court og public oponion? Tz public is still behind, most believing in myths, superstition,...so do not worry about them. Or u r not tough?

    ReplyDelete
  7. Ni kwa sababu majipu yamekuwa mengi na yameachwa kwa muda mrefu. Pole.
    Wahusika waache kuandika taarifa zisizo na uthibitisho.

    ReplyDelete
  8. Ajiangalie? Kwa nini? Mbona bongo kuna za roho korosho nyingi tu. Msisahau methali isemayo hasidi hana sababu zaidi ya husuda. Na ukiwa juu basi ni smaku ya husuda. Kwa nini sasa? Ndo muda nchi ina wasomi wengi watokao vyuo duni. Yawezekana watu wengi hivi wakawa mahasidi? Ndio na zaidi yawezekana dunia nzima wakawa wakosefu. Kwa wale wafuatao dini za islam na kristo, watu wa nuhu-noa waliangamizwa dunia nzima kwa ukosefu ikiwamo kwa nini nuhu ndo awe muhubiri wakati wao ni matajiri na wasomi na wajanja nk. Husuda hiyo. Watu wa lot. Watu wa...na hizo zilikuwa nchi nzima.

    ReplyDelete
  9. Ndiyo. Watu wapuuzi wanahisi anajidai. Hivi kujidai au kujiona au kunata au kuwa na sura nzuri kama ya baba ni kosa la jinai nba ngapi hapa.

    ReplyDelete
  10. Nimebarikiwa kuzidi watu wengi walio karibu yangu (wafanyakazi wenzangu, jirani zangu, ndugu zangu). Nakwambia mpaka nawaepuka. Kila mmoja kuna juhudi ya kunishughulikia wakati mimi huwasaidia. Eengine nkiwasaidia waona najidai. Nlishaacha. Kikulacho ki nguoni mwako.

    ReplyDelete
  11. Mheshimiwa Ridhiwan,

    Pole wala hukuwa na sababu wala haja ya kuwajibu hao watu.

    Wamejaa povu kinywani. Kikubwa wewe kaa kimya, wakati ni dawa pekee ya jeraha lolote, yatakwisha tu! Hayo unayoyaona hovi sasa ni wivu tu, na watu kukosa mambo ya maana kufanya.

    Badala ya kutafuta riziki zao wamekaa kuangalia nani kabahatika na kuaanza kumsakama.

    Usiwajali. Hao ni kama kumbikumbi wana msimu wao na baadaye mabawa yatang'ooka na watatambaa tu. YATAKWISHA TU!

    ReplyDelete
  12. Mdau wa UK umenichekesha , eti Rizwani kashika nafasi za juu serikalini kwa miaka 25 unajua ana umri gani? hebu piga hesabu halafu ndio uendelee kuandika. Sidhani hata 40 yrs kafika Uongo mwingine muuache jamani kha!

    ReplyDelete
  13. Mchangiaji nambari tatu hapo juu unajiita mdau wa UK acha acha kuwadharau wanawake. "wivu wa kikie" unadhani ungekua hapo ulipo kama si mwanamke unayemdharau?

    ReplyDelete
  14. Mchangiaji wa mwisho acha feminism baki kwenye mada.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...