Mkurugenzi Mtendaji wa
Zantel, Benoit Janin akizungumza na waandishi juu ya mipango ya kampuni yake
ikiwamo kuzindua mtandao wa 4G upande wa Zanzibar.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Zantel akijibu maswali ya waandishi katika mkutano huo. Kushoto
kwake ni Rachel Samren, Mwenyekiti wa Bodi ya Zantel na kulia ni Cynthia
Gordon, Mkurugenzi Mtendaji wa Millicom Upande wa Afrika.
Mwenyekiti
wa Bodi, Rachel Samren akizungumza na waandishi wa habari. Katikakati ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Zantel, Benoit Janin na kulia ni Cynthia Gordon,
Mkurugenzi Mtendaji wa Millicom Upande wa Afrika.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Zantel katika mkutano huo.
Kampuni
ya Millicom leo imetangaza kuanza utekelezaji wa mpango wake wa uwekezaji
katika kampuni ya Zantel, ambao utajumuisha uboreshaji wa huduma na mtandao wa
kampuni hiyo.
Akizungumza baada ya mkutano
wa kwanza wa bodi ya Zantel tangu Millicom iliponunua asilimia 85% ya hisa za
Zantel, Mkurugenzi Mtendaji wa Milicom upande wa Africa, Cynthia Gordon,
alisema maboresho hayo yatajajikita katika kuimarisha kwa huduma za simu, intaneti, pamoja ambayo
yatapelekea Zantel kutoa huduma bora na ya uhakika.
'Millicom
itajikita katika kuiwezesha Zantel kukuza na kuboresha ukuaji na upanuzi wa shughuli zake hapa nchini ili kuifanya
Zantel iendelee kuongoza soko la Zanzibar na kuendelea kutoa huduma zenye ubunifu zaidi pamoja na kuongeza wigo wa
kuwafikia wateja wengi zaidi’ alisema Gordon.
Kampuni ya Millicom pia
imeelezea nia yake ya dhati ya kuimarisha ushirikiano wake na Serikali ya Zanzibar,
ambayo pia anamiliki asilimia 15% ya hisa za Zantel katika kuhakikisha kampuni
inakuwa msitari wa mbele katika kuwajengea uwezo na kuboresha maisha ya watu wa
Zanzibar.
'Kama kampuni
inayoongoza Zanzibar, ushirikiano wetu na serikali ya Zanzibar una umuhimu wa
kipekee, na katika hili, Millicom itahakikisha wananchi wa Zanzibar
wanawezeshwa kupitia miradi mbalimbali ya kijamii’ alisema Rachel Samren,
Makamu wa Rais, Mambo ya Nje wa Millicom.
Pia akizungumza
katika mkutano huo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Zantel, Benoit Janin alisema kampuni
ya Zantel pia itazindua mtandao wa kwanza kabisa wa 4G kwa Zanzibar ambao una
lengo la kuimarisha nafasi yao kama kampuni inayoongoza katika huduma za
intaneti pamoja na kuimarisha upatikanaji wa huduma za mtandao kwa wakazi wa
Zanzibar.
‘Zantel itafaidikia
moja kwa moja na uzoefu pamoja na utamaduni wa ubora wa Millicom, hivyo
kuhakikisha Zantel inaingia katika zama mpya za kuboresha bidhaa zake na kuongeza
ubora wa huduma ikiwemo huduma za kifedha kwa njia ya simu ya mkononi na
kupanua maeneo ya ushirikiano katika miradi ya kijamii’ alisema Benoit.
Benoit ambaye hivi
karibuni alitembelea wafanyakazi upande wa Zanzibar, amesema amejionea namna
walivyo na ari ya kushirikiana na uongozi mpya wa Zantel katika kuhakikisha
kampuni yao inaendelea kuongoza Zanzibar.
Kuanzia mwanzoni mwa
mwaka 2016, Zantel pia itafanya uzinduzi wa huduma za kusisimua ikiwa ni pamoja
na kupanuliwa kwa huduma za 3G na 4G na pia kuboresha huduma za kifedha kwa njia ya simu ili kuifanya
Zantel kufikia malengo yake katika utoaji wa huduma kwa jamii.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...