Mshindi  wa shindano la Mama shujaa wa Chakula 2015, Linaloendeshwa na Shirika la Oxfam kupitia program yake ya Grow msimu wa nne Caroline Chelele amekabidhiwa zawadi ya vifaa vya kilimo vyenye thamani ya kiasi cha shilingi Millioni 20, nyumbani kwake kata ya Ifakara mkoani Morogoro.

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano hayo ya zawadi  Mkoani Morogoro wilayani  Kilombero kata ya Ifakara,Meneja Ushawishi na Utetezi kutoka Shirika la Oxfam,Eluka Kibona alisema zawadi hiyo ni moja ya utekelezaji wa shindano hilo kwa mshindi aliyeshinda shindano hilo la Mama shujaa wa Chakula 2015.

Alisema shirika lao linatoa takribani Milioni 20 kwa mshindi ambapo mshindi  anatakiwa kuchagua zawadi ya vifaa vya kilimo ili kuweza kumuwezesha zaidi. Kibona alisema Mshindi huyo alikabidhiwa Pawatila kwa ajili ya kubebea Mazao,vifaa vya umuagiliaji pamoja na Shamba lenye Ekali 7. "Huu ni muendelezo wa shindano la mama shujaa wa Chakula kukabidhi zawadi kwa ajili ya kuwainua wakulima wadogo wadogo kuonekana na Serikali kama wao wanamchango mkubwa kwa jamii kutokana na Chakula wanacholima ndicho kinacholisha taifa,"alisema Kibona . Aliongeza shindano hilo lipo chini ya Kampeni ya GROW yenye lengo la kuwainua wakulima wadogo wanaokumbana na changamoto mbalimbali katika kilimo.

Kwa Upande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Kilombero , Yahya Naniya aliishukuru shirika hilo kwa hatua ya kuwathamini na kuwapigania wakulima wadogo ambao asilimia kubwa kati yao ni wanawake.Alisema  kupitia shindano hilo linaweza kuongeza Chachu kwa wakulima kufanya  shughuli za kilimo kwa kasi na kuongeza wigo mpana wa kupata mazao mengi kutokana na Mashirika mbalimbali kuwawezesha.

Naye Mshindi wa Shindano hilo 2015,Caroline Chelele alisema  atahakikisha zawadi hizo anazifanyia kazi ipasavyo itakayomuwezesha kumuongezea mazao mengi zaidi. Aliomba Serikali pamoja na mashirika mbalimbali kuendelea kuasidia wakulima wadogo na kuhakikisha nao wanathaminiwa kama wakulima wakubwa.
Mshindi wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula Msimu wa nne Bi. Caroline Chelele aliyekaa kwenye Pawatila akifurahia zawadi zake, Muda mfupi baada ya kukabidhiwa.
 Katibu Tawala wa Wilaya ya Kilombelo Bw. Yahya Naiya (wa pili kushoto) aliye muwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Kilombelo akikata utepe kuashiria tukio la kumkabidhi zawadi rasmi mama shujaa wa chakula msimu wa nne 2015 Bi. Caroline Chelele, wa kwanza kushoto ni Mercy Minja Kaimu mkurugenzi wa wa mji wa Ifakara, wa tatu kutoka kulia ni Mama Shujaa wa Chakula Bi. Caroline Chelele na Mbunge wa Jimbo la Kilombelo Mh. Peter Lijuakali
 Katibu Tawala wa Wilaya ya Kilombelo Bw. Yahya Naiya (wa pili kushoto) aliye muwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Kilombelo akimpongeza Mama shujaa wa chakula 2015 baada ya kukabidhiwa zawadi ya vifaa vya kilimo vyenye thamani ya Tsh Milioni Ishirini(20,000,000)

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...