Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi ya Mkoani Iringa imeibuka mshindi wa kwanza kimkoa na kushika nafasi za juu kikanda na kitaifa, kati ya Halmashauri tano za Mkoa wa Iringa, baada ya kufanya vizuri zaidi wakati wa mbio za mwenge wa uhuru ulipokimbishwa Mkoani Iringa mnamo mwezi Juni mwaka huu.   

Taarifa ya kitengo cha habari na mawasiliano cha Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi imevitaja baadhi ya vigezo kati ya vigezo 10 vilivyoshindanishwa, kuwa ni pamoja na miradi yenye maslahi kwa umma iliyozinduliwa wakati wa mbio za mwenge wa uhuru, uimarishaji wa vikundi vya uzalishaji mali kwa wanawake na vijana.

Vigezo vingine vinavyozingatiwa ni pamoja na mapambano dhidi ya Malaria, dawa za kulevya, michango ya Mwenge wa uhuru sanjari na mapokezi ya mwenge wenyewe ulipowasili wilayani Mufindi

Akizungumzia ushindi huo, Mkuu wa wilaya ya Mufindi JOWIKA KASUNGA amewashukuru wakazi wa Mufindi na wadau wa maendeleo kwa michango yao na akatoa rai ya kundelea kuuenzi mewenge wa uhuru kama alama na utambulisho wa taifa.

Aidha, taarifa hiyo imezitaja nafasi ilizoshika kuwa ni ushindi wa kwanza kimkoa, ushindi wa 05 kwa kanda ya kiuchumi yenye zaidi Halmashauri 36 pamoja na nafasi ya 22 kitaifa ikijumuisha zaidi ya Halmashauri 140.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...