Baadhi ya Maofisa wa Jeshi la Magereza waliohudhuria katika hafla ya kuaga mwili wa Marehemu Mkaguzi wa Magereza, Morice Peter.
Mke wa Marehemu Mkaguzi wa Magereza, Dorice Peter(kulia) akipewa msaada ndugu wa karibu wakati wa kusindikiza mwili kuelekea kwenye gari tayari kwa safari ya kuelekea Mkoani Morogoro kwenye mazishi.
Mkaguzi wa Magereza, Seleman Sued wa Gereza Kuu Ukonga, Jijini Dar es Salaam akisoma Wasifu wa Mkaguzi wa Magereza Morice Peter aliyefariki juzi Desemba, 2015 katika Hospitali ya Dar Group, Jijini Dar es Salaam.
Ndugu na jamaa waliojitokeza kuuaga mwili wa Marehemu Mkaguzi wa Jeshi la Magereza, Morice Peter aliyekuwa akihudumu katika Gereza Kuu Ukonga, Jijini Dar es Salaam. Mkaguzi Morice Peter amefariki juzi Desemba 22, 2015 baada ya kuugua muda mrefu katika Hospitali ya Dar Group Jijini Dar es salaam
Maafisa wa Jeshi la Mageereza wameubeba mwili wa Marehemu Mkaguzi wa Magereza, Morice Peter wakiuingiza nyumbani kwake kabla ya kutoa heshima za mwisho leo Desemba 24, 2015 katika Viwanja vya Gereza Kuu Ukonga Jijini Dar es Salaam.Picha na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...