Aliyewahi kuwa nahodha wa Yanga na Timu ya Taifa (Taifa Stars) Ally Mayay Tembele alikuwa ni miongoni mwa wahitimu zaidi ya 800 waliotunukiwa shahada za uzamili katika fani mbalimbali kutoka katika Chuo kikuu cha Mzumbe kampasi ya Dar es salaam .
Katika sherehe hizo za mahafali ya 14 ya Chuo kikuu cha Mzumbe Kampasi ya DSM zilizofanyika katika ukumbi wa mikutano wa J.K.Nyerere jijini Dar es salaam, Tembele alitunukiwa Shahada ya Uzamili katika Sayansi ya Masoko(Msc Marketing management).
Aidha, akiongea na Michuzi blog, Mayay alitoa wito kwa wanamichezo na wasanii kujiendeleza kielimu katika fani mbalimbali ili kuweza kukabiliana na changamoto mbalimbali zikiwemo zile zilizomo ndani ya fani zao
Mayay ambeye ni Afisa Biashara katika Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji ni mchambuzi wa soka katika vituo vya redio na televisheni na pia ni kocha mwenye leseni daraja C kutoka Shitikisho la soka baranai Afrika (CAF).
Ally Mayay akiwa na mwanae Yumnah baada ya kulamba nondozzzz zake
Ally Mayay na msanii wa muziki wa kizazi kipya Gwamaka Kaihula (King crazy GK) ambao wote wamelamba nondozzz ya shahada ya uzamili katika chuo kikuu cha Mzumbe
Well done you Tembele, From Simba damu
ReplyDelete