Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu wakati alipokuwa anawasili Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam kwa ziara ya kikazi. Waziri Kitwanga alifanya mazungumzo na Viongozi Wakuu wa jeshi hilo na kukubaliana kuweka mikakati zaidi ya kukabiliana na uhalifu nchini.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kumaliza mazungumzo na Viongozi Wakuu wa Jeshi la Polisi nchini. Waziri Kitwanga aliwaambia waandishi wa habari kuwa, wamekubaliana na Viongozi Wakuu wa jeshi hilo kuweka mikakati zaidi ya kukabiliana na uhalifu nchini. Wapili kushoto meza kuu ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu. Wapili kulia meza kuu ni Naibu IGP, Abdulharam Kaniki. Kulia ni Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa Jeshi hilo, Paul Chagonja. Kushoto meza kuu ni Kamishna wa Polisi Jamii nchini, Mussa Ali Mussa. Kushoto ni Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi, Suleiman Kova.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati aliyekaa), Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu (watatu kulia waliokaa) wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Wakuu wa Jeshi la Polisi nchini mara baada ya kikao chao kilichofanya katika Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Jeshi hilo kumalizika. Waziri Kitwanga alifanya mazungumzo na Viongozi hao na kukubaliana kuweka mikakati ya kupambana na uhalifu.
Picha
zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
WAZIRI wa Mambo Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga amesema njia ya kudhibiti dawa za kulevya kuingia nchini ni kuweka mfumo wa kisasa wa kudhibiti uingiaji dawa hizo, kuwa na orodha ya waingizaji wa dawa ni kazi bure kutokana na kukosa mamlaka ya kisheria.
Kitwanga ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati alipokutana na Maafisa Wakuu wa Jeshi la Polisi, amesema katika kukabiliana na uingizaji wa dawa za kulevya ni kuweka mfumo imara na jeshi la polisi lazima lijipange katika udhibiti huo.
Kitwanga amesema kuwa mfumo wa kiteknolijia ukiwekwa hautabagua mtu yeyote au mkubwa katika madaraka awe mdogo wakishajulikana watachukuliwa hatua za kisheria bila kuangaliwa nafasi walizo nazo.
“Orodha ya wauza unga ukiwanayo haitasaidia na kufanya hivyo ni kuhisi, lakini huna sheria ya kuweza kuwabana katika orodha hiyo” amesema Kitwanga.
Kitwanga amesema kuwa katika mambo waliyojpanga nayo na jeshi la polis ni kuhakikisha wanaimarisha ulinzi katika bandari ili kuweza kudhibiti utoroshaji wa vitu mbalimbali ambavyo vinatoka bila utaratibu.
Hata hivyo amewataka polisi watu washitakiwe kwa kesi walizo nazo na sio kuwabambikia watu wasio na hatia kusababisha kufungwa kwa kesi zisizowahusu.
Kitwanga amesema utoroshaji wa madini,jeshi la polisi haliwahusu wakihitajika na Wizara ya Nishati na Madini watafanya hivyo katika kukabiliana na utoshaji huo.
Aidha amesema kati ya askari 45,000 ni askari 10,000 ndio wenye makazi hivyo wanatarajia kujenga nyumba 5000 ikiwa nia nia askari wote kukaa katika makambi ni rahisi kuweza kuhitajika kwa muda wowote.
SI KWELI. HII YAKO NI NON-STARTER KWENYE VITA YA MADAWA YA KULEVYA.
ReplyDeleteORODHA INAKUSAIDIA KUANZA KUWAPELELEZA WAHUSIKA KUJUA MALI WALIZO NAZO NA NAMNA WALIVYOZIPATA. UTAKUTA MTU ANA KIBANDA KIDOGO CHA BIASHARA LAKINI ANA MAGHOROYA NA MA RANGE ROVER NA HAKUNA ANAYEJIULIZA AMEPATAJE. SASA MTU KAMA HUYU WEWE WAZIRI UKIPEWA JINA LAKE UTAKAA KIMYA TU USUBIRI USHAHIDI (WAKATI MHUSIKA ANASHIRIKIANA NA MAMLAKA HUSIKA KUKWEPA MKONO WA SHERIA?). KINACHOTAKIWA WEWE NI KUWEKA MAKACHERO KUCHUNGUZA WATU KAMA HAWA. WAFANYABIASHARA WAKUBWA WA MADAWA (SI WADOGO WADOGO) HAWAZIDI 50, SASA MNASHIDWA KUFUATILIA NYENDO ZAO?
NCHI ZIKIZOENDELEA KAMA MAREKANI WAKISHAKUWA NA HISIA ZA WAZI LAKINI HAWANA USHAHIDI, WANATAFUTA NJIA NYENGINE YA KUWAKAMATA HAWA WATU: WANAWASHITAKI KWA MAKOSA YA KUKWEPA KODI SABABU WAUZA MADAWA WENGI HAWALIPI KODI SABABU WANAPENDA KUFICHA VIPATO VYAO! NDIO MAANA UNAKUTA SUSPECTS WENGI WA MADAWA YA KULEVYA WANAFUNGWA KWA MAKOSA YA KUTOLIPA KODI. KITENGO CHA KUPAMBANA NA MADAWA YA KULEVYA TANZANIA NI MOJA YA VITENGO VINAVYOTAKIWA KUWA REVAMPED, KAMA ‘TAKUKURU’.
WAZIRI INABIDI USE CREATIVE NA U-THINK OUTSIDE THE BOX. HIZO KAULI ZA KUSEMA MAJINA HAYAKUSAIDII NDIO ZILIZOTUFIKISHA HAPA. HIZO NI KAULI ZA KUFANYA KAZI KWA MAZOEA. KAMA MTU ANATAJWA NA WATU WENGI HATA WEWE WAZIRI UNAWEZA KUMFUATA NA KUZUNGUMZA NAYE AKUELEZE NI KWANINI WATU WANAMTAJA TAJA. HIYO TU ITASAIDIA HUYO MHUSIKA KUOGOPA KUENDELEA KU-DEAL NA MADAWA! NA ASKARI WANAOTAJWA TAJWA UWACHUNGUZE MAISHA YAO NA MALI ZAO NA UWAITE KUWAULIZA NI KWA NINI WANATAJWA TAJWA. HII WIZARA NAONA INGEMFAA MZEEE MWENYEWE WA ‘HAPA KAZI TU’.
Basi mainfoma na makachero wa nini? Si lazima upate pa kuanzia kiongozi?
ReplyDelete"Mfumo imara wa jeshi la polisi" Usituchanganye afande
Si kazi ya waziri kukamata au kupeleleza au kupata kizibiti. Majina yawasaidie polisi wenyewe. Waziri aambiwe wote wako ndani na vizibiti vipo.
ReplyDeleteWaziri kafanya vizuri kukataa majina na katoa jibu zuri. wao kama polisi wana ushahidi wowote? wamefanya upelelezi kama majukumu yao yalivyo? Hivi hiyo ni kasi ya JPM? Yaani wakiona wahalifu wakimbilie kuripoti kwa waziri ili awakamate. Hizi si taratibu za polisi kama ilivyo kwenye PGO.
ReplyDeleteNingekuwa waziri ningeyapokea hayo majina na nkawaambia polisi "ntawapigia simu hawa jamaa nwaulize kama kweli ni wadawa."
Kuyakataa hayo majina, yawe ya kweli au si ya kweli haihusu hapa. Yeye kama waziri wa majeshi yote, KIUTENDAJI inabidi ayapokee, ayafanyie kazi ya awali ya uchunguzi ...somewhere to start.
ReplyDeleteAwakabidhi wahusika, ambao YEYE ndio waziri wao, YEYE AFUATILIE
Hatutaki majibu mafupifupi rahisi rahisi ambayo yanapelekea kujiuliza maswali mengi zaidi