Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa
Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Dkt. Tonia Kandiero Ikulu Jijini Dar
es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuelekeza jambo Mwakilishi Mkazi wa
Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Dkt. Tonia Kandiero Ikulu Jijini Dar
es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mwakilishi Mkazi wa Benki
ya Maendeleo ya Afrika AfDB Dkt. Tonia Kandiero Ikulu Jijini Dar es
Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi wa Rwanda hapa
nchini Eugene Kayihura aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Rwanda hapa
nchini Eugene Kayihura aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo. Picha
zote na IKULU
![]() |
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. amemuhakikishia Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo
ya Afrika Dkt. Tonia
Kandiero kuwa Serikali yake ya Awamu ya Tano itaendelea kushirikiana na benki
hiyo katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Dkt. Magufuli
amesema hayo leo Tarehe 21 Desemba, 2015 Ikulu Jijini Dar es Salaam, alipokutana
na kufanya mazungumzo na Mwakilishi huyo.
Pamoja na kumhakikishia
ushirikiano Rais Magufuli ametoa wito kwa benki hiyo kupunguza michakato ya
kuelekea katika utekelezaji wa miradi na badala yake ameshauri uwepo utaratibu
wa haraka unaowezesha kuanza kwa miradi katika kipindi kifupi baada ya fedha
kutolewa.
Kwa upande wake
Dkt. Tonia Kandiero pamoja na kumpongeza Rais Magufuli kwa kuchaguliwa kwake
kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika awamu ya tano, amemhakikishia
kuwa benki iko tayari kuendelea kushirikiana na Tanzania katika maendeleo kama
ambavyo imekuwa ikifanya na kwamba kwa sasa imetenga dola Bilioni mbili nukta
tatu kwa ajili ya kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo.
Ameongeza kuwa
katika mipango yake ADB imelenga kujielekeza katika utoaji wa mikopo katika
sekta ya nishati na usafiri.
Naye Rais Magufuli
ameipongeza ADB kwa kuamua kujielekeza katika sekta hizo za nishati na usafiri
na pia ameisisitiza kuangalia namna itakavyounga mkono mradi wa ujenzi wa reli
ya kati kwa kiwango cha kisasa yaani standrd gauge.
Katika hatua
nyingine Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na
kufanya mazungumzo na Balozi wa Rwanda hapa nchini Mh Uegene Sagore Kayihura
Ikulu Jijini Dar es salaam.
Kwa upande wake
Rais Magufuli amemuhakikishia Balozi Kayihura kuwa serikali yake ya awamu ya tano
itaendelea kushirikiana na Rwanda ili wananchi wa nchi zote mbili waweze
kunufaika kimaendeleo.
Katika mazungumzo
hayo Balozi Kayihura amewasilisha salamu za pongezi kutoka kwa Rais Paul Kagame
wa Rwanda ambaye amempongeza Rais Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa awamu
ya tano wa Tanzania.
Balozi Kayihura
amesema Rais Kagame amefurahishwa na hatua ambazo Rais Magufuli anazichukua
hasa katika usimamizi na utendaji kazi wa bandari na kumhakikishia kuwa Rwanda
iko tayari kushirikiana na Tanzania hasa kuitumia bandari ya Dar es salaam
ambayo hupitisha asilimia zaidi ya 70 ya mizigo ya Rwanda.
Ameongeza kuwa
Rwanda na Tanzania ni nchi marafiki na majirani hivyo kuna kila sababu ya
kujenga ushirikiano madhubuti katika sekta ya uchumi.
Rais Magufuli
amemuomba Balozi Kayihura kumfikishia Rais Kagame salamu za shukrani kwa
kumpongeza kuchaguliwa kuwa rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
na kwamba amedhamiria kuimarisha zaidi ushirikiano na Rwanda.
Gerson
Msigwa
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
21 Desemba,
2015
|
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...