Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemalizia kujaza nafasi za uteuzi wa
Mawaziri na Naibu Waziri alizobakiza wakati akitangaza baraza la
Mawaziri la kwanza katika utawala wake wa awamu ya tano.
Uteuzi huo ni kama ifuatavyo;
![]() |
Dkt. Joyce Ndalichako – Ameteuliwa kuwa Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi. (Ni baada ya kumteua kuwa Mbunge) |
![]() |
6. Prof. Makame Mbarawa – Amehamishwa kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji na kwenda Wizara ya Ujenzi, uchukuzi na Mawasiliano |
![]() |
Mheshimiwa Hamad Masauni – Ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi |
![]() |
Profesa Jumanne Maghembe – Ameteuliwa kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii. |
![]() |
Dkt. Philip Mpango – Ameteuliwa kuwa Waziri wa Fedha na Mipango (Ni baada ya kumteua kuwa Mbunge). |
Katika hatua nyingine Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewatakia heri watanzania wote katika Sikukuu za Maulid, Christmas na Mwaka Mpya na kuwataka washerehekee kwa amani na utulivu.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
23 Desemba, 2015
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...