maa1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha  Maalim Seif Sharif Hamad ,Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Ikulu jijini Dar es Salaam na kufanya  Mazungumzo kuhusu hali ya kisiasa ya  Zanzibar. Katika Mazungumzo hayo viongozi wote wamefurahishwa na hali ya usalama na utulivu inayoendelea.
maa2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Maalim Seif Sharif Hamad ,Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Ikulu jijini Dar es Salaam.Rais amemshukuru  Maalim Seif  na amemsihi waendelee na mazungumzo hadi suluhisho la muufaka lipatikane.
maa3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Maalim Seif Sharif Hamad ,Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Ikulu jijini Dar es Salaam, wakwanza kushoto ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan.
maa4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha  na Maalim Seif Sharif Hamad ,Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amekutana naMakamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mgombea Urais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharrif Hamad, leo tarehe 21 Desemba, 2015 Ikulu Jijini Dar es Salaam  kufuatia maombi yake ya siku nyingi.

Mazungumzo ya Viongozi hao pia yamehudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Viongozi hawa kwa pamoja wamejadili hali ya kisiasa Zanzibar na wamefurahishwa na hali ya usalama na utulivu inayoendelea. Aidha, Mhe. Rais Magufuli amewapongeza Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Kwanza wa Rais  wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, na viongozi wote wanaoshiriki katika mazungumzo ya kuleta hali ya uelewano Zanzibar. 

Rais Magufuli pia  amewapongeza na kuwashukuru wananchi wa Zanzibar kwa kudumisha amani na utulivu wakati wa mazungumzo baina ya viongozi wa CUF na CCM yakiendelea huko Zanzibar. 

Katika Mazungumzo hayo Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Maalim Seif Sharrif  Hamad amemueleza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania juu ya hali ya siasa Zanzibar kadiri anavyoielewa yeye na Rais Magufuli amemshukuru Makamu huyo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kwa taarifa yake nzuri huku akimsihi waendelee na mazungumzo hadi suluhisho muafaka lipatikane. 

Majadiliano yanayoendelea yanatoa fursa ya kudumishwa kwa utulivu na sifa njema ya nchi yetu. Wote kwa pamoja wamewaomba wananchi waendelee kuwa watulivu ili kutoa nafasi ya majadiliano yanayoendelea kufikia hatma njema. Wameelezea matumaini yao kuwa vyama vya CCM na CUF haviwezi kushindwa kupata suluhu ya mgogoro huo. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemuhakikishia kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano itahakikisha kuwa amani na utulivu unaendelea kudumishwa Zanzibar. 

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU. 

21Desemba, 2015

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Namkumbusha Maalim ule usemi wake safari hii hakuna kunong'onezwa. Wafanye watakavyofanya ila haki yako upewe, mara ya nne hii.Tatu zote umewaachia kwa nia njema ya kuilinda heshima nchi. Ebu na wao safari hii wafanye kama unavyofanyaga.....hahahahahaha kama wataweza ...

    ReplyDelete
  2. Amani na utulivu viwe ni kwa ajili ya haki na maendeleo. Hapa tulivyonavyo vinamlinda mvunja haki na mpinga demokrasia. Na meenye haki hathubutu kusema.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...