Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa Japan
nchini Masaharu Yoshida aliyefika Ikulu Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mazungumzo.
Katika Mazungumzo hayo Balozi Yoshida amempongeza Rais Magufuli kwa kuchaguliwa
kuiongoza Tanzania katika awamu hii ya tano na pia amezungumzia miradi
mbalimbali inayofadhiliwa na Japan hapa nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa
Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mmoja wa Maofisa walioambatana na
Balozi Yoshida Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Kalenda kutoka kwa Balozi
wa Japan hapa nchini Mheshimiwa Masaharu
Yoshida mara baada ya kumaliza mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...