
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli amemtumia salamu za
rambirambi Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye
amepatwa na msiba mzito wa kufiwa na Dada yake Mpendwa Bi. Tausi Khalfan
Kikwete kilichotokea jana tarehe 17 Desemba, 2015 huko nchini India.
Katika
salamu hizo, Rais Magufuli amesema anaungana na familia ya Rais Mstaafu Kikwete
katika kipindi hiki kigumu cha majonzi ya kuondokewa na mtu muhimu kwa familia."Kwa
masikitiko makubwa nakupa pole nyingi Mheshimiwa Rais Mstaafu Dkt. Jakaya
Kikwete kwa kufiwa na dada yako ambaye alikua nguzo muhimu katika familia"
Amesema Rais Magufuli.
Aidha
Rais Magufuli amemuomba Rais Mstaafu Kikwete kumfikishia salamu nyingi za pole
kwa familia nzima na amewaomba wawe na moyo wa subira na uvumilivu katika
kipindi hiki kigumu.Rais
Magufuli amemuomba Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema aipumzishe roho ya marehemu
Tausi Khalfan Kikwete mahali pema peponi, Amina.
Imetolewa
na;
Gerson
Msigwa
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
18 Desemba, 2015
Rest in peace
ReplyDelete