Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za
rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza kufuatia ajali ya basi la
kampuni ya New Force kugongana na lori, na kusababisha vifo vya watu 12, na
wengine 15 kulazwa Hospitali.
Ajali
hiyo imetokea tarehe 18 Desemba, 2015 Majira ya saa nane mchana katika Kijiji
cha Mahenge, Wilaya ya Kilolo Mkoani IRINGA ambapo Basi la kampuni ya New Force
lenye namba T 483 CTF lililokuwa limebeba abiria 49 limegongana na Lori la
Kampuni ya Reign-ford Limited lenye namba T 616 BEF na Tela lake lenye namba T
320 DEF lililokuwa na shehena ya mbao .
Rais
Magufuli amemuomba Mkuu huyo wa mkoa kufikisha salamu za pole kwa familia,
ndugu, jamaa na marafiki wote ambao wamepoteza ndugu zao katika ajali hiyo
mbaya"Nimesikitishwa
sana na kutokea kwa ajali hii, ninawapa pole nyingi wote waliopoteza ndugu zao
na ninawaombea Majeruhi wote wapone haraka ili waungane na familia zao na
kuendelea na shughuli zao za maendeleo" amesema Rais Magufuli.
Amewaombea
marehemu wote kwa Mwenyezi Mungu ili azipumzishe roho zao mahali pema peponi,
Amina.Aidha
Dkt. Magufuli ametoa wito kwa watuaji wote wa barabara hususani madereva kuwa
waangalifu waendeshapo vyombo vya usafiri na amewakumbusha wananchi wanaotumia
barabara kwa kusafiri ama kusafirisha mizigo kutoa ushirikiano kwa vyombo
husika pale wanapobaini kuwepo vitendo ambavyo ni chanzo cha ajali.
Imetolewa
na; Gerson Msigwa,
Kaimu Mkurugenzi wa
Mawasiliano, IKULU
18 Desemba, 2015
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...