Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akibadilishana mawazo na Rais wa
China, Mheshimiwa Xi Jinping pembezoni mwa Mkutano wa Africa na China
unaofanyika Johannesburg , Afrika Kusini. Waliosimama pembeni ni Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Tanzania, Rais Thomas Boni Yayi wa Benin, Rais
Filipe Nyusi wa Msumbiji na Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini.
----------------------------------Taasisi ya Commonwealth Partnership for Technological Management (CPTM) inayojishughulisha na kukuza ushirikiano katika nyanja ya sayansi na teknolojia kwa nchi za Jumuiya ya Madola, imemtunuku Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete, heshima ya Juu ya CPTM (Companion Award) kwa kutambua mchango wake katika kuhamasisha ukuaji wa matumizi ya sayansi na teknolojia ikiwemo matumizi ya huduma za fedha kwa njia ya simu. Rais Mstaafu Kikwete, alikabidhiwa Tuzo hiyo tarehe 1 Desemba, 2015.
Taasisi hiyo yenye makao makuu yake London ndio inayoendesha Midahalo ya Kimataifa maarufu kama Smart Partnership Dialogue. Mkutano wa mwisho wa aina hiyo ulifanyika Dar es Salaam mwaka 2013 ukiwa Na kali mbiu ya "Kutumia Teknolojia Kuchochea Maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii Barani Afrika".

Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete aliteuliwa na Mama Nkosamana Dlamini Zuma kuwa Mjumbe Maalum wa AU Comoro. Mhe. Kikwete alikwenda Moroni, Comoro tarehe 30 Novemba, 2015 kufanya mikutano na wadau wa siasa kuhusu mgogoro wa kisiasa unaonukia nchini humo kuhusu mchakato wa uchaguzi mkuu wa nchi hiyo utakaofanyika April, 2016
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...