Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, Amos Makalla, akiwa ameshika glasi ya kinywaji kwa ajili ya kufurahia kwa pamoja kwenye hafla ya kuwapongeza walimu wa wilaya ya Hai mkoani humo baada ya kupata matokeo mazuri katika ufaulu wa darasa la saba mwaka huu. Hai imeshika nafasi ya kwanza kiwilaya mkoani humo na nafasi ya nne kitaifa.

Na Mwandishi Wetu, Hai
MKUU wa Mkoa Kilimanjaro, Amos Makalla, amehudhuria halfa ya kuwapongeza walimu wilayani Hai, mkoani humo, kwa kufanikisha ufaulu mzuri wa darasa la saba. Wilaya ya Hai imepata nafasi ya kwanza kiwilaya mkoani Kilimanjaro, huku ikishika ikishika nafasi ya nne kitaifa, jambo lililomkuna Mkuu huyo wa Mkoa Kilimanjaro.
Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro Amos Makalla, mwenye suti nyeusi akiingia katika hafla hiyo, wilayani Hai, mkoani Kilimanjaro.

Akizungumza katika halfa hiyo akiwa kama mgeni rasmi, RC Makalla, alisema kwamba Hai wanastahili pongezi na wanapaswa kuendelea kufanya bidii ili wazidi kufaulisha kiwilaya na kitaifa. Alisema kuna haja ya sekretarieti ya Mkoa huo na Halmashauri zote kujipanga na kushughulikia kero za walimu, madai ya mishahara, kupandishwa kwa madaraja pamoja na kujibu barua zao kwa wakati ili kuwapa moyo walimu wao hao.

“Mkoa wetu unawapa pongezi kubwa walimu wote wa wilaya ya Hai kwa kufanya kazi kubwa na nzuri ya kuhakikisha kwamba wanafunzi wenu wanafaulu vizuri. “Naomba muendelee kujituma katika ufundishaji wenu, huku nikiahidi ushirikiano mkubwa katika ofisi yangu na kwenu ninyi walimu ili kuleta ushirikiano mkubwa kati yetu,” alisema.

RC Makalla amekuwa akifanya ziara mbalimbali mkoani Kilimanjaro ili kuongeza ufanisi katika majukumu yao ya kila siku, huku wakiitumia vyema falsafa ya Hapa Kazi Tu, inayotumiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr John Pombe Magufuli.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Ben Toronto.December 04, 2015

    kwani hao wageni ktk hiyo shughuli hawaezi kutembea ktk ardhi ya kawaida ya muumba mpaka wawekewe zulia jekundu !! huu ni ujinga usio na kifani....watu kazi kujikuza tuuuuuu !!!

    ReplyDelete
  2. we nawe ungekaribishwa wewe usingepita zulia jekundu? kwani zulia wanapita liko hewani au juu ya ardhi ya muumba? acha chuki binafsi hiyo ndio raha ya kusoma sio kukimbia umande.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...