MWIMBAJI nguli wa muziki
wa Injili barani Afrika, Rebecca Malope ambaye ni raia wa Afrika Kusini
anatarajia kuongeza nguvu katika Tamasha la Krismasi linalotarajia kufanyika
Desemba 25 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha
hilo, Alex Msama muimbaji huyo atakuwa jukwaa moja na wenzake Sarah K wa
Kenya na Ephraim Sekeleti wa Zambia ambao watafikisha shukrani za
Watanzania baada ya kufanya uchaguzi Mkuu kwa amani na utulivu, uchaguzi
uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu.Msama alisema Kamati yake inaendelea na mchakato wa
kufanikisha tamasha hilo ambalo ni muendelezo wa Tamasha la Amani lililofanyika
Oktoba 4 uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Aidha Msama alisema Watanzania walichukilie tamasha hilo
kama sehemu ya kurudisha shukrani kwa Mungu baada ya kutupitisha katika kipindi
kigumu cha uchaguzi Mkuu ambao ulifanyika kwa amani na utulivu ingawa kulikuwa
na viashiria vya uvunjifu wa amani.
Msama alisemAa waimbaji wa Tanzania watakaosindikiza tamasha
hilo ni pamoja na Rose Muhando, Upendo Nkone, Joshua Mlelwa, Kwaya ya
Wakorintho wapili huku kamati ikiendelea na mchakato wa kufanikisha tamasha
hilo.
“Tumejipanga vilivyo na tamasha la Krismasi, hivyo
tujiandae kupiga goti la kumrudishia Mungu Shukrani baada ya uchaguzi Mkuu
ambao ulikuwa na mguso wa aina yake kutoka kwa vijana walioonesha kutaka
maendeleo kutoka kwa serikali,” alisema Msama.Naye mjumbe wa Kamati ya maandalizi ya Tamasha hilo, Khamis
Pembe aliwahakikishia Watanzania watakaohudhuria tamasha hilo ulinzi wa uhakika
kupiia Jeshi la Polisi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...