Wizara
ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo inakanusha taarifa zilizoandikwa katika gazeti
la Mwananchi la tarehe 24.12.2015 yenye
kichwa cha habari “JPM kutolipa makocha Stars”.
Serikali kupitia Wizara inayohusika na michezo haijatoa
tamko la kutowalipa makocha
wanaofundisha timu ya Taifa Stars kama ilivyoripotiwa na gazeti hilo.
Suala
la malipo ya makocha wa Taifa Stars linashughulikiwa kwa mujibu wa sheria na taratibu
za Serikali, pindi maamuzi yatapofikiwa, serikali itatoa maelekezo kama
itaendelea kuwalipa au la.
Serikali
ya Awamu ya Tano inathamini michezo yote ikiwemo mpira na miguu , kwa hiyo
itaendelea kushirikiana na Vyama vya vyote vya michezo na wadau wote wa michezo
kwa ujumla katika kuhakikisha kuwa michezo inaimarika na kuwa chanzo cha ajira
kwa vijana nchini.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI (MAELEZO)
24 DESEMBA, 2015
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...