
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angeline Mabula
wakati alipotembelea Shirika la Nyumba la Taifa(NHC).
wakati alipotembelea Shirika la Nyumba la Taifa(NHC).
Angeline amesema kuwa shirika la nyumba la Taifa linajenga nyumba kwaajili ya kuuzwa pamoja na kupangisha na si kuwapa wanchi bure.
Amesema kuwa gharama ya kujenga nyumba hizo inakuja katika maandalizi ya ujenzi ikiwa ni pamoja na kuandaa miundombinu kama Barabara, Maji pamoja na Umeme.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa(NHC), Nehemia Mchechu amesema shirika hilo tayari limejenga nyumba za kutosha katika miji mikubwa kama Dar es Salaam, Arusha na Mwanza.
Pia amesema katika nyumba za mikoani shirika hilo limeuza nyumba hizo kwa 40% hadi 50% huku akisisitiza zaidi kuendelea na Kampeni ya (Nyumba yangu, Maisha yangu) ili wananchi wawezi kumudu gharama za nyumba hizo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...