Serikali imeamua muda wowote kuanzia mwezi huu kuanza ukaguzi wa vibali vya Ajira za Wageni nchini, kufuatia muda wa siku 14 kuisha uliotolewa na serikali katika tangazo la utolewaji wa vibali vya kazi kwa wageni nchini lililotiwa saini Desemba 14, mwaka huu, na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Aiira, Vijana na Watu wenye ulemavu), Jenista Mhagama (Mb), ambaye aliwataka waajiri wote nchini kwa muda wa siku hizo wawe wametekeleza matakwa ya Sheria ya Kuratibu Ajira za Wageni nchini Na. 1 ya Mwaka 2015.

“Katika taarifa tuliyoitoa mwezi huu, tuliwajulisha waajiri wote wenye waajiriwa wageni ambao wana vibali vya kazi za muda (Carry on Temporary Assignment) na wale wote wasiokuwa na vibali vya ajira vilivyotolewa na kamishna wa kazi nchini kuwa wanatenda kosa. Kamishna wa kazi amepewa mamlaka kutoa vibali vya ajira kwa wageni wanaotaka kufanya kazi nchini. Hivyo hakuna mamlaka nyingine yoyote inayoruhusiwa kutoa vibali vya ajira kwa wageni,” amesema Mhagama.

Amesema hayo, Tarehe 29 Desemba, 2015, Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na kikosi maalum kitakachoendesha operasheni hiyo chenye wajumbe kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Uhamiaji na Wakala wa Usalama na Afya mahali pa kazi (OSHA), ikiwa lengo ni kufuatilia kama agizo lililotolewa na serikali limefuatwa na kuhakikisha taratibu zinazopaswa kufuatwa katika utoaji wa vibali vya ajira zinazingatiwa.

“Serikali ilitoa muda wa siku 14 kwa waajiri wote wawe wametekeleza matakwa ya Sheria Na. 1 ya mwaka 2015 vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.” Alisitiza Mhagama.

Mwezi Machi, mwaka huu Bunge la 10 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha Sheria ya Kuratibu Ajira za Wageni nchini Na. 1 ya Mwaka 2015 (The Non-Citizens (Employment Regulation) Act)). Sheria imeanza kutumika rasmi tangu tarehe 15 Septemba, 2015. Sheria hiyo inaanzisha Mamlaka moja yautoajiwa vibali vya ajira kwa wageni na Mamlak ahiyo ni Kamishna wa Kazi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye ulemavu), Bibi. Jenista Mhagama (Mb), akifuatilia maelezo ya wajumbe wa kikosi Maalum cha kukagua vibali vya Ajira za Wageni (hawapo pichani) wakati alipokutana nao Jijini Dar es Salaam tarehe 29 Desemba, 2015, (katikati) ni Naibu Waziri (Kazi, Ajira na Vijana), Anthony Mavunde na Katibu Mkuu (kazi na Ajira), Eric Shitindi.
Baadhi ya wajumbe wa kikosi maalum cha kukagua vibali vya Ajira za Wageni kutoka Idara ya Uhamiaji nchini na Wakala wa Usalama na Afya mahali pa kazi (OSHA), wakifuatilia maelekezo ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye ulemavu), Bibi. Jenista Mhagama (Mb) (hayupo pichani), wakati walipokutana naye Jijini Dar es Salaam tarehe 29 Desemba, 2015.
Katibu Mkuu (kazi na Ajira), Eric Shitindi akieleza jinsi operasheni ya Kukagua vibali vya Ajira za wageni kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye ulemavu), Bibi. Jenista Mhagama (Mb) (hayupo pichani) wakati alipokutana na wajumbe wa kikosi maalum cha kukagua vibali hivyo Jijini Dar es Salaam tarehe 29 Desemba, 2015.
Baadhi ya wajumbe wa kikosi maalum cha kukagua vibali vya Ajira za Wageni kutoka, Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Uhamiaji nchini na Wakala wa Usalama na Afya mahali pa kazi (OSHA), wakifuatilia maelekezo ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye ulemavu), Bibi. Jenista Mhagama (Mb) (hayupo pichani), wakati walipokutana naye Jijini Dar es Salaam tarehe 29 Desemba, 2015.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Tunashukuru sana kwa serekali kuliona hili lakini,mimi naona kuna mapungufu makubwa sana kwenye hili la kuunda kikosi kazi kufuatilia vibali vya wageni wanaofanya kazi hapa nnchini.Kwanza ni matumizi mabaya ya kodi zetu kwa hakuna kitu watakacho kuja kikitoa mbele ya jamii zaidi ya kutudhalilisha wafanyakazi wazawa,pili,hawa wajumbe waishia kuhongwa na matajiri na kufanya kama matakwa yao.mie nafikiri njia bora ambayo ingeleta manufaa kwa taifa ni kwa waziri husika kutoa anuani zake zote eg.email,sanduku la posta na physical adress na pia simu zote,na kuwataka wananchi wenye taarifa kamili wazipeleke kwake na hapo ndo angepata kujua ni kampuni ipi haijatimiza matakwa ya sheria.Kwa kufanya hivi pesa za umma zitakuwa zimelindwa na si hili la kuunda kikosi kazi kinachohitaji pesa za umma.

    ReplyDelete
  2. SAFI SANA WAZIRI NAOMBA MWENDE KAMPUNI YA KIOO LIMITED ILIYOKO CHANGOMBE MUJIONEE MAAJABU

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kiongozi Mimi napenda uende mwenyewe hususani kwenye makampuni ya uchimbaji wa Madini( migodini) huku tunapata taabu sana wazawa.

      Delete
  3. The mdudu, Mama toka mwenyewe ofisini achana na mambo ya vikosi kazi watahongwa hao na Mafisadi au ukipenda waite matajili kwa mwendo huo mama sijui kama utaenda sambamba na Kasi ya Magufuli #hapakazitu hili eneo ni nyeti na ndio uti wa kazi za watanzania so lazima Mama na msaidizi wako lazima muwe Serious na tough decision

    ReplyDelete
  4. Ndugu waziri,pamoja na nia nzuri ulionayo lakini,mbinu zitakuangusha kwani hawa watu uliowaweka kwenye kikosi kzi ndo hao hao waliohusika na kutoa vibali,sasa hapa huoni kesi ya nyani hakimu kuwa ngedere??la msingi ni kuwata watu wa idara ya kazi,uhamiaji, na watu wa TIC wakupatie majina ya watu waliowapatia vibali,baada ya kupata ndo hapo sasa utazame wewe mwenyewe au kamishina wa kazi na kujua uhalali wake na si vinginevyo.

    ReplyDelete
  5. Kaka michuzi kuhusu hili la wageni kufanya kazi ambazo watanzania Twaweza zifanya au kwa maana nyingine hazitaji TX,mie nakushauri ufungue Ukurasa rasmi kwa sie wazalendo kutoa maoni na majina ya wageni na kampuni wanzafanya kazi na pia kazi wazifanyazo.Ukifanya hili uatakuwa umetundea haki sie wanyonge kwa utakuwa ndo mdomo wetu,ambapo wewe utamfikishia ujumbe Waziri kwa urahisi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...