
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na waandishi wa
habari kuhusiana na hatua zilizofikia katika kutatiua mgogoro baina ya
Timu ya Stand Unite ya mjini Shinyanga na kamati ya uendeshaji ya timu
hiyo iliyopo chini ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa leo jijini Dar es
Salaam.Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,WHUSM.

Baadhi ya wajumbe wa kamati ya
utendaji ya timu ya Stand United ya mjini Shinyanga wakifuatilia maelezo
ya Waziri wa Habaroi, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses
Nnauye (hayupo pichani) wakati wa kikao baina yao na Waziri huyo leo
jijin Dar es Salaam.


Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo (kushoto)akifuatilia maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa
timu ya Stand United Bw. Aman Vicent (katikati)wakati wa kikao baina ya
wajumbe wa Kamati tendaji ya Club hiyo na Mhe. Waziri ili kujadili
mgogoro unaoikabili timu hiyo leo jijini Dar es Salaam.
………………………………………………………………………………………….
Na: Frank Shija, WHUSM.
Serikali imeagiza kumalizika kwa
mgogoro uliopo baina ya Timu ya mpira wa miguu ya Stand United na Kamati
ya uendeshaji wa timu hiyo iliyopo chini ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Agizo hilo limetolewa leo jijini
Dar es Salaam na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape
Moses Nnauye mara baada ya kumaliza kikao na uongozi wa Stand United.
Nape amesema kuwa imefika wakati
vilabu vikapewa uhuru wa kujiendesha kwa kutumia katiba zao badala ya
kingiliwa na chombo kingine chenye maslahi binafsi.
“Wizara itasaidia kuona mgogoro
huu unaisha kwa Stand United kupewa uhuru wa kujiendesha yenyewe na
uongozi uliokuwapo kupewa mamlaka yake ya kusimamia na kuendesha
shughuli za Timu yao kwa mujibu wa Katiba”
Aidha aliongeza kuwa Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kusimamia uendeshaji wa mchezo wa mpira
wa miguu kwa kuzingatia sheria ,kanuni na taratibu za mchezo huo ili
kuepuka migogoro isiyokuwa na tija.Kwa upande wake Mwenyekiti wa
Timu ya Stand United Bw. Aman Vicent ameishukuru Serikali kupitia Wizara
yenye dhamana na masuala ya michezo kwa kuona umuhi wa kushughulikia na
kumaliza mgogoro wao.
Aman amesema kuwa kutokana na
makubaliano waliyofikia katika kikao hicho imani yao ni kuwa suala hili
litamalizika mapema kwa kuwa Waziri mwenye dhamana ameonyesha nia na
utayari wa kuhakikisha suala hili linaisha kwa wakati ili Timu iweze
kusonga mbele katika kujiletea maendeleo.
Kikao baina ya Waziri na uongozi
wa Timu hiyo kimefanyika ikiwa ni matokeo ya juhudi za uongozi wa Timu
ya Stand Uinted kuinusuru timu yao baada ya kujikuta katika mgogoro
usiokuwa na tija zaidi ya maslahi binafsi kutoka na udhamini walionao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...