SERIKALI imewaagiza maafisa wa afya nchini kuhakikisha kila kaya inakuwa na choo bora ikiwa ni hatua ya kuhakikisha jamii inaepekana na magonjwa yanayotokana na uchafu mazingira , sambamba na suala la usafi wa mazingira kuwa endelevu kama ilivyoagizwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Aidha Serikali imepiga marufuku ulaji wa matunda yaliyomenywa barabarani.
Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Donan Mmbando(Pichani),wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo.
Katibu Mkuu huyo ambaye alikuwa ameambatana na baadhi ya viongozi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais na Ofisi ya Waziri Mkuu, wakiwemo wa wizara yake kwa ajili ya kuzungumzia mambo matatu ambayo ni suala la usafi wa mazingira katika kuadhimisha siku ya Uhuru ,Desemba 9, mwaka 2015, ugonjwa wa kipindupindu na polio.
“Wakuu wa mikoa na wilaya wanatakiwa kutekeleza agizo hili kwa kujiwekea utaratibu wa kufanya usafi maeneo yao,” alisema Dkt. Mmbando.
Dkt. Mmbando alisema ikumbukwe kuwa ugonjwa wa kipindupindu pamoja na magonjwa mengine yanayohusiana na uchafu huenea kwa kasi kutokana na hali duni ya usafi katika maeneo tunayoishi. Hivyo takwimu zinaonesha kuwa kati ya taka ngumu zinazozalishwa ni 50% tu huzolewa na kupelekwa dampo. Kiasi cha taka kinachobaki huzagaa katika maeneo mbalimbali hususani kando kando ya barabara, katika maeneo ya kukusanyia taka (Collection points), chini ya madaraja na katika maeneo ya wazi hali inasayobabisha miji yetu kuonekana michafu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...