Serikali imesema kuwa ina taarifa ya wahitimu wa Taasisi ya Maendeleo ya Maji (WDMI),kukosa nafasi za ajira hivyo suala hilo limefanyiwakazi na serikali kwa kushirikiana na wadau wengine wa maji hivyo wawe na uhakika wa kuajiriwa na wasibweteke wakipata hizo fursa kwani hakutakuwa na nafasi kwa wazembe au wasiowajibika. 
Akizungumza wakati wa mahafali ya saba ya taasisi hiyo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam juzi, Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mbogo Mfutakamba alisema ukosefu wa ajira kwa wahitimu hao ni kilio cha muda mrefu na yeye na serikali wanakitambua. 
“Tunakitambua kilio hicho, tunafahamu umuhimu wa maji kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa Taifa hasa kipindi hiki ambapo Taifa limejielekeza katika miradi mikubwa ya kilimo cha umwagiliaji” alisema na kuongeza kuwa licha ya wahitimu kutegemea serikali lakini pia wadau wengine sasa wamehusishwa. 
”Serikali yetu hivi sasa haina mambo ya mchakato au sijui vitu gani isipokuwa jambo ambalo ninawahakikishia ni kuwa changamoto hiyo imefanyiwakazi kwa kuwashirikisha wadau wengine na kwa wale ambao mtapata nafasi muende mkafanyekazi kwani kwa sasa hakuna lugha nyingine isipokuwa kazi tu” alisema. 
Alibainisha kuwa chuo hicho kina umuhimu wa pekee katika maendeleo ya nchi hususan kipindi hiki ambacho kumekua na mahitaji makubwa ya maji kwa ajilio ya shghuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na kilimo cha umwagiliaji. 
Alisema hatua ya chuo hicho kudahili wanafunzi wa program ya maji shahada ya kwanza fani ya Uhandisi wa Maji na Umwagiliaji inapaswa kuungwa mkono na serikali kwa kukiwezesha chuo kutimiza malengo yake na pia kuwahakikishia wahitimu ajira. 
“Tuna upungufu mkubwa wa watalaam wa maji hivyo serikali imehakikisha mnapata ajita” alisema na kuongeza kuwa mpango wa ujenzi wa jengo la ghorofa sita kwa ajili ya chuo hicho upo hatua za mwisho na wakati wowote utekelezaji wa mradi utaanza. 
Katika risala yao kwa mgebni rasmi wahitimu hao pamoja na mamo mengine walilalamika uchakavu wa majengo, uhaba wa vifaa vya kujifunzi na ukosefu wa maabara za kutosha na maktaba ikiwa ni pamoja na chumba cha kompyuta.
 Wahitimu katika Taasisi ya Maendeleo na Usimamizi wa Maji (WDMI), wakiwa katika maandamano kuelekea katika mahafali ya saba ya taasisi hiyo, jijini Dar es Salaam juzi. Jumla ya wahitimu 288 walitunukiwa Astashahada na Stashahada  katikia sekta ya maji.

 Wahitimu katika Taasisi ya Maendeleo na Usimamizi wa Maji (WDMI), wakiwa katika maandamano kuelekea katika mahafali ya saba ya taasisi hiyo, jijini Dar es Salaam juzi. Jumla ya wahitimu 288 walitunukiwa Astashahada na Stashahada  katikia sekta ya maji.

 Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mbogo Mfutakamba akizungumza wakati wa mahafali ya saba ya Taasisi ya Maendeleo ya Usimamizi wa Maji (WDIM), jijini  Dar es Salaam juzi. Jumla ya wahitimu 288 walitunukiwa Astashahada na Stashahada  katikia sekta ya maji.

 Sehemu ya wahitimu katika Taasisi ya Maendeleo na Usimamizi wa Maji (WDMI), wakiwa katika maandamano kuelekea katika mahafali ya saba ya taasisi hiyo, jijini Dar es Salaam

 Burudani ya ngoma ya asili ya Zanzibar

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...