
Mkurugenzi
wa Shirika la Nyumba NHC Bw. Nehemia Mchechu Kyando akizungumza na
wageni waalikwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa uuzaji wa nyumba za mradi
wa 711 uliopo Kawe jijini Dar es salaam, Nyumba hizo ziko kwenye
majengo 7 yenye ghorofa 11 kila moja ambayo yanatarajiwa kuchukua watu
1000 kwa na huu ni utangulizi wa ujenzi wa mji mpya wa kisasa
unaotarajiwa kujengwa eneo la Tanganyika Pakers Kawe jijini Dar es
salaam ambao ukikamilika utaweza kuchukua watu 15000.
Watu
wanaohitaji kununua nyumba hizo wanatakiwa kufika ofisi za NHC
Kinondoni au Makao Makuu ya Shirika la Nyumba NHC Upanga au wanaweza
kutembelea kwenye mtandao wa shirika hilo kwa maelezo zaidi ili kununua
nyumba hizo hafla ya uzinduzi wa nyumba hizo ilifanyika mwishoni mwa
wiki katika makao makuu ya shirika hilo Upanga.

Mkurugenzi
wa Shirika la Nyumba NHC Bw. Nehemia Mchechu Kyando akizungumza na
wageni waalikwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa uuzaji wa nyumba za mradi
wa 711 uliopo Kawe jijini Dar es salaam. 

Meneja
wa Masoko na Mauzo wa NHC, Tuntufye Mwambusi akizungumza na Monica
Joseph Mkurugenzi wa Kampuni ya Monifinace Investment Group Limited
wakati wa uzinduzi huo.

Meneja
wa Masoko na Mauzo wa NHC, Tuntufye Mwambusi akimsikiliza Bw. David
Shambwe Mkurugenzi wa Fedha Maendeleo ya Biashara NHC katika uzinduzi
huo kulia ni Mwita Makenge Mkurugenzi wa Kampuni ya Wegmar Limited na
kushoto ni William Genya Meneja Maendeleo ya Biashara NHC .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...