Watu wawili wamejeruhiwa vibaya na kulazwa katika hospitali ya wilaya ya Nzega,huku sababu kuu ikielezwa kuwa ni wivu wa mapenzi:https://youtu.be/SjQN8nQ-GSQ
Wakati watu wengine wakifungua zawadi za siku kuu wengine wapigana na kupelekwa hospitali hii leo : https://youtu.be/CNiEYQDX9NI
Askofu mkuu wa kanisa la KKKT mkoa wa Ruvuma amewataka wakristo kuchunga midomo yao ili kuepuka mifarakano:https://youtu.be/EZhmGAqYE2M
Vijana nchini Tanzania wahimizwa kuanzisha viwanda vidogo vidogo na kuacha kuagiza bidhaa kutoka nchi za nje: https://youtu.be/PNsBQT224uo
Bondia maarufu Thomas Mashali amefanikiwa kulipiza kisasi na kuibuka mshindi baada ya kumtwanga mangumi Francis Cheka:https://youtu.be/kdQGmITQ_qc
Idadi ya watu waliofariki katika ajali ya lori mkoani Tanga, yaongezeka na kufikia 5 baada ya majeruhi mwingine kufariki hii leo.https://youtu.be/iA6uhiGFGCE
Wajawazito na watoto katika hospitali ya wilaya ya Maswa waelezwa kulazimika kulala wawili wawili katika kitanda kimoja kutokana na ufinyu wa wodi huku wakitoa rai kwa serikali Kufungua majengo ya wodi mpya zilizokamilika. https://youtu.be/4UGrJ-XO5ns
Serikali ya watu wa China yafadhili mradi wa maji safi katika wilaya ya Lindi na kuondoa kero kubwa iliyokuwa ikiwakabili wananchi kwa muda mrefu.https://youtu.be/F-ihrtUSTWg
Afya za wakazi wa Tabora zaelezwa kuwa hatarini kufuatia hali ya uchafu uliokithiri katika soko kuu la manispaa hiyo. https://youtu.be/JRtSDMDmJQM
Wakazi wa kata ya Mwandege wilayani Mkuranga mkoani Pwani watakiwa kuwa subira ili sheria ifuate mkondo wake baada ya mwekezaji mwenye asili ya Asia kuchukua kimabavu maeneno yao na kuharibu mazao yao.https://youtu.be/kRp5DMTSkvU
Wananchi wa manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma wafanya usafi katika maeneneo mbalimbali wakishirikiana na vikosi vya ulinzi na usalama.https://youtu.be/V079o04KIEg
Waziri wa nishati na madini Prof. Sospeter Muhongo awataka wananchi wa jimbo lake kuanzisha mfuko maalum wa kushughulikia maendeleo ya elimu badala ya kuitegemea serikali katika kila jambo. https://youtu.be/VinS-UwKh_Y
Maafisa maliasili wilaya ya Bukombe mkoani Geita walalamikiwa kukamata ng’ombe wa wafugaji zaidi ya 1000 na kuwafungia zizini kwa muda wa siku 5 bila malisho. https://youtu.be/ripm4lZ_qqU
Mwanadiplosia wa muda mrefu na katibu mkuu mstaafu wa umoja wa nchi huru za Afrika OAU asema mgogoro wa Burundi umelitia doa bara la Afrika.https://youtu.be/T-1yySKbwsA
Wafanyabiashara wa matunda ya jumla katika soko kuu la matunda mkoani Kigoma waiomba serikali kupitia SIDO kujenga viwanda vya usindikaji matunda ili kuepusha hasara wanayoipata kwa matunda kuoza.https://youtu.be/QKwcO_bGuUo
Wakulima wa zao la maharage machanga mkoani Arusha waiomba serikali kuwasidia kupata soko la uhakika wa zao hilo kwa kuwaandalia mfumo rasmi wa kukutan na wateja moja kwa moja. https://youtu.be/XI2cOiVEdFE
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...