Tatizo Gani Kula Nyama
Je! Ni kawaida asili ya mwanaadam kuwa nakula nyama? Kufuatana na mafunzo ya sanaa ya Yoga, inashauri sana kuepuka madhara yanayosababishwa na athari ya kula nyama ambayo ni mjadala mrefu na uanaleta hoja nyingi katika maisha ya mfumo mzima wa sanaa hiyo.
Leo, kama tunajiandaa kuelekea mwaka mpya 2016 na malengo mapya, basi moja ya ushauri na mazungumzo ni kufahamishana na kuhusu mambo kazaa ya sanaa ya Yoga na uhusiano wake wa kutokula nyama kiafya.
Mfumo wa kuchanganya na kuyeyusha chakula wa binaadam “ Digestive system” pamoja na jinsi meno na maumbo yaliyo kunatofauti sana kulinganisha na wale walao nyama kiasilia “Carnivorous”, wanatofauti kubwa kama vile maumbile ya mfumo wao wa chakula tumboni. Tumbo lao“Bowel” ni fupi mara tatu tu ya urefu wa mwili wao. Hii inawaruhusa kuweza kutoa mabaki ya chakula chao cha nyama mwilini haraka sana kwa ufupi huo wa utumbo. Hivyo wadudu wa “Bacteria” hawakai muda mrefu tumboni na kutoka kupitia mfumo wa haja kubwa.
Utumbo wa “Carnivorous” unauwezo mara 10 zaidi ya kemikali ijulikanayo kama “Hydrochloric Acid” kulinganisha na wale wasiao kula nyama kisilia kama vile wanyama wanao kula majani tu, na huwawezesha wala nyama kuchanganya na kuyeyusha nyama mbichi na hata mifupa bila taabu yeyote. Meno yao pia ni ushahidi dhahiri, “ Canines” meno yalioyochongoka na marefu kuwawezesha kumudu hali ya ulajiwao wa nyama.
Binaadam, ni wazi kabisa sio mlaji nyama asilia “ Natural”. Maumbile ya mfumo wao wa kuchanganya na kuyeyusha chakula “Digestive system”, unadhihirisha hivyo. Ni aina zote za mazao ( Maharage, kunde, mbaazi, soya) ya aina mbali mbali, matunda karanga aina zote ni vyakula ambavyo asili ya mwanaadam tokea enzi na enzi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...