Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Tume ya Nguvu za Atomiki, Tanzania, Dr. Mwijarubi Nyaruba aliekaa katikati pamoja na wataalamu wa Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya namna ya kukabiliana na kuimarisha ulinzi wa matukio ya kinyuklia.
Tume ya Nguvu za Atomiki, Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani wanaendeshesha mafunzo ya namna ya kukabirina na matukio ya mionzi hatari, mafunzo haya yatachukua siku nne na yameanza jana jumatatu tarehe 07 disemba na yatafika ukomo wake tarehe 10 disemba, 2015, mafunzo haya yana jumla ya washiriki 23 kutoka katika nchi sita za ukanda wa Afrika ikiwa ni Uganda, Kenya, Zimbabwe, Botswana, Ethiopia, Namibia na mwenyeji Tanzania mafunzo yanalenga zaidi kutoa mwongozo jinsi ya kukabiliana na majanga yanayoweza kusababishwa na mionzi hatari ya nyuklia endapo hakutakuwa na uangalizi wa kutosha.
Akifungua mafunzo haya jijini Arusha, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki, Tanzania Dr. Mwijarubi Nyaruba amesema, kutokana na kukua kwa kasi kwa teknolojia duniani ni muhimu sana kwa nchi wanachama wa shirika la nguvu za atomiki duniani kuendelea kutoa mafunzo na kujadiliana jinsi ya kukabiliana na majanga yanayoweza kusababishwa na mionzi ayonisha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...