Mwanamuziki Kasongo Mpinda Clayton (anayeimba) ametutoka leo jioni baada ya kuugua kwa muda mrefu. Kasongo atakumbukwa kama mwimbaji mwenye sauti ya kipekee toka alipoibukia ghorofa ya saba pale New Africa Hotel jijini Dar es salaam akiwa na MK Group, wana Ngulupa Tupa Tupa na baadaye Maquis du Zaire 'Wana Kamanyola' akikonga nyoyo washabiki wa muziki, na baadaye Wazee Sugu chini ya King Kikii.
Badhi ya nyimbo zilizompandisha chati Marehemu Kasongo ni 'SEYA' , 'ANGELOU', 'MUME WANGU MWENYEWE' na 'NSONONEKA' katika mtindo wa 'Ogelea piga mbizi' . Cheza hizo video nne umsikie Kasongo Mpinga....
Marehemu Kasongo anatarajiwa kuzikwa kesho saa 10 Kinondoni. Msiba upo nyumbani kwake Kinondoni karibu na jengo lenye Benki ya Akiba Commercial Bank jijini Dar es salaam.
Marehemu Kasongo anatarajiwa kuzikwa kesho saa 10 Kinondoni. Msiba upo nyumbani kwake Kinondoni karibu na jengo lenye Benki ya Akiba Commercial Bank jijini Dar es salaam.
Inna Lillahi wa Inna Ilayhi Rajiuun.
ReplyDeleteDah......chozi lanidondoka , R.I.P LEGENDARY
ReplyDeleteRIP Kasongo Mpinda. Hizi nyimbo nilikuwa nazikia sana nilivyokuwa mtoto ila nilikuwa sijui mwimbaji ni nani. Asante sana kwa kunikumbusha mbali. Naimisi RTD kipindi cha jambo na mchana mwema bila kasahau chaguo lako na club raha leo shooo! Na wakati umewadia wa salamu za wagonjwa hosipitalini leo tunawapa pole. Ajuae bwana Mungu kwa mzima kuwa mfu mgonjwa kuwa salama leo tunawapa pole. Dah!
ReplyDelete