Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi jijini Mbeya, mapema mchana wa leo wamekamata bidhaa zilizoingizwa nchini kimagendo kupitia mpaka wa Tunduma. Bidhaa hizo ni vinywaji aina ya Dragon vilivyokuwa vikisafirishwa na gari aina ya Toyota Hiace. Pichani ni Kamanda wa Polisi Mkoani wa Mbeya, SACP Ahmed Msangi (akiwasiliana kwa njia ya simu) akiwa pamoja na Afisa wa TFDA Kanda ya Nyanda za juu kusini, Peter Namaumbo.
Na Deo Kakuru, Mbeya
MAMLAKA ya Chakula na Dawa TFDA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini imekamata katuni 185 za vinywaji vya kuongeza nguvu mwilini DRAGON vinavyotengezwa Afrika ya Kusini na bidhaa nyingine zenye thamani ya Zaidi ya shilingi milioni 7 zilizoingizwa nchini kimagendo kupitia mpaka wa Tunduma.
Bidhaa hizo zimekamatwa zikiwa zimepakiwa kwenye gari lenye No za usajili T622CRT aina ya Toyota Hiace zilizokuwa zikitokea Tunduma kuletwa Mbeya mjini kwa ajili ya matumizi ya binadamu.
TFDA imeshindwa kuzitambua bidhaa hizo ambapo kwa mujibu wa mamlaka hiyo bidhaa yoyote inayoingia nchini inatakiwa kusajiliwa ili kupata uhalali wa watumizi yake ili kubaini kama hazina madhara kwa binadamu.
Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Ahmad Msangi amethibitisha kukamatwa kwa bidhaa hizo na kueleza kuwashikilia dereva na utingo wake huku harakati za kumtafuta mmiliki wa bidhaa hizo Veronica Tweve zikiendelea.
Dereva wa gari hilo Julius Mwankusi yuko chini ya ulinzi lakini anashangaa kutomuona tajiri yake akija kumuwekea dhamana.
Kukamatwa kwa bidhaa hizo ni mwendelezo wa msako unaofanywa kwa siri na jeshi la polisi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali lengo likiwa ni kukomesha upitishwaji wa bidhaa za magendo katika maeneo ya mipakani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...