Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi Umma Bw.Peter Mushi (wa pili kushoto) akizungumza alipokuwa akiendesha mkutano kwa njia ya video na Sekretarieti ya Mkoa wa Mara jana jijini Dar es Salaam (watatu kulia) ni Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi Umma Bw. Leonard Mchau .
Baadhi ya watendaji kutoka wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakiendelea na Mkutano kwa njia ya Video na Sektertarieti za Mikoa ya Lindi,Mara,Geita,Singida na Shinyanga jana jijini Dar es Salaam.
Mwandishi wa Habari kutoka kituo cha Televisheni cha ITV Bw. Hendry Mabumo akimuuliza swali Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao Bw.Charles Senkondo ambaye hayupo katika picha jana jijini Dar es 


Na Anna Nkinda–Maelezo
WATANZANIA wametakiwa kutumia technolojia ya mawasiliano ikiwemo kufanya mikutano kwa njia ya video ambayo itawaondolea gharama ya kusafiri na hivyo kuokoa fedha  na muda.

Rai hiyo imetolea   hivi karibuni na Mkurugenzi Mtendaji wa TaGLA Charles Senkondo wakati akiongea na waandishi wa habari wakati wa mkutano wa kazi wa video conference kati ya Ofisi ya Rais  Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Taasisi zake, Sekretarieti za mikoa na Mamlaka za Serikali za mitaa.

Senkondo alisema kufanya mikutano kwa njia ya video kunamfanya mtu asisafiri na hivyo kuepukana na ajali, kutopoteza muda awapo safarini na na kupata wasaa wa  kukaa na familia yake.

“Kuanzishwa kwa TaGLA kumeongeza uwezo wa kufanya kazi kwa ubunifu zaidi, kwa njia ya kisasa, kwa maamuzi zaidi ya kiuendeshaji kwa kuangalia kila mara mahitaji ya wadau na kutumia mbinu za soko katika utoaji wa huduma bora”.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...