
Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akiongea na Uongozi wa Mkoa wa
Tanga,Waziri Ummy yupo mkoani Hapa kwenye ziara ya kikazi sehemu ya
afya na wazee.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais
(Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora),Seleman Jaffo(Kulia) na Katibu
Tawala wa Mkoa wa Tanga,Salum Chime kwenye ukumbi wa Mkuu wa Mkoa,

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto akisaini kitabu cha wageni kwenye Ukumbi wa Mkuu wa mkoa.

Waziri Ummy Mwalimu akiwa na Mkuu
wa Wilaya ya Tanga Abdullah Lutari (wa pili Kulia) na afisa toka wizara
ya afya Dkt.Ibrahim Maduhu.
………………………………………………………..
Na. Catherine Sungura,WAMJW-Tanga
Halmashauri zote nchi zimetakiwa kujitahidi kudhibiti upoteaji
wa dawa na vifaa tiba kwenye vituo vya afya ili wananchi waweze kupata
tiba sahii na inayostahili Hayo yamesema leo na Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati alipokutana na Uongozi
wa Mkoani hapa.
Ummy alisema kumekuwa na upoteaji dawa na vifaa tiba mara
vifikapo kwenye vituo vya afya kwa kuzunguka na kupelekwa kuuzwa kwenye
maduka ya dawa na hospitali binafsi.
Alimtaka Mganga mkuu wa mkoa kudhibiti upoteaji wa dawa kwa
kutoa elimu kwa kamati ya afya juu ya majukumu yao ili dawa zote
zinazowafikia zisipotee mikononi mwa watu wachache.“Nimejifunza kuwa dawa zinapopokelewa kwenye vituo zinazunguka
tena na kwenda kwa wauzaji binafsi hivyo hakuna udhibiti wa uingiaji na
utokaji wa dawa na hivyo kufanya dawa nyingi kupotea kwenye maduka ya
dawa binafsi
Aidha alisema ataongea na Bohari ya dawa (MSD) ili kuanzisha
utaratibu wa kila dawa zinazopelekwa kwenye kituo ziwe zinabandikwa
kwenye ubao wa matangazo wa vituo vyote nchini ili wananchi wajue dawa
zilizopo kwenye kituo chake nia aina gani.
Hata hivyo amemuomba Naibu Waziri, Ofisi ya
Rais(Tamisemi,Utumishi na Utawala Bora),Seleman Seleman Jaffo
kuwachukulia hatua pamoja na kusisitiza suala la nidhamu,uwajibikaji na
uadilifu kwa watendaji hususan kwenye sekta ya afya, kwakuwa yeye hana
dhamana ya kuwasimamisha kazi moja kwa mojaWaganga wakuu wa mikoa na
Wilaya kwakuwa yeye anasimamia sera na miongozo ya sekta ya afya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...